Your are here: Home // Habari // WASANII WA FILAMU WAPO NYUMA- MH. MDEE.

WASANII WA FILAMU WAPO NYUMA- MH. MDEE.

Mh. Halima Mdee

Mh. Halima Mdee Mbunge wa Jimbo la Kawe.

MHESHIMIWA Halima Mdee Mbunge wa Jimbo la Kawe ameeleza kuwa wasanii wa filamu pamoja na kuwa na muonekano katika jamii lakini wapo nyuma sana katika masuala ya kijamii, lakini jambo baya kuliko yote ni kukosa umoja na ushirikiano katika masuala yao, hilo ameligundua katika kuugua kwa msanii mwenzao Juma Kilowoko ‘Sajuki’.

Mh. Halima Mdee

Mh. Halima Mdee Mbunge wa Jimbo la Kawe aliyewaasa wasanii kujitenga.

“Wasanii wa filamu wapo nyuma sana kila mtu anajijali yeye tu hana msaada kwa mwenzake, leo hii Sajuki anaumwa na alikuwa akihitaji msaada wa kifedha ili akatibiwe nje ya Nchi lakini hakuna hata msanii mmoja aliyefanya juhudi zozote hata kuchangisha fedha hizo, tatizo lilomkuta Sajuki si tatizo la pekee yake mtu yoyote linaweza kumkuta,”anasema Mh. Mdee.

Mbunge huyo mwenye mvuto Bungeni na mpiganaji katika masuala ya kijamii alitoa pongezi kwa kundi la Orijino Komedi kwa kubuni na kuvunja vipindi vyao na kutumia muda huo kuchangisha fedha kwa ajili ya kumsafirisha mgonjwa, pia anasema kuwa wao wanajitahidi kuibana Serikali Bungeni kuhusu maslahi yao na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo alitoa ahadi kuongelea maslahi ya wasanii katika bajeti mwezi wa saba.
.

Wema Sepetu

Wema Sepetu alishiriki wimbo wa Mboni Yangu.

Mh. Halima Mdee katika kuguswa na ugonjwa wa msanii Sajuki pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya msanii huyo, pia aliungana na wasanii wa muziki sambamba na Waheshimiwa Wabunge katika kuimba wimbo maalumu kwa ajili ya kumchangia msanii Sajuki huku wasanii wa filamu wakiwa wachache ambao walikuwa ni William J. Mtitu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Wema Sepetu na Wastara Juma pekee.
.

Juma Kilowoko

Sajuki msanii wa filamu Swahiliwood anayehitaji matibabu

Hali hiyo ambayo hata waheshimiwa wamaeanza kuiona ni tatizo, ni wazi wanawatetea watu walio katika makundi yasiyo na manufaa kwa wasanii wenyewe na jamii nzima kwa ujumla hivi sasa kuna kundi la TAFF na Bongo Movie Unity ni kundi gani linawakilisha maslahi ya wasanii wote kwa ujumla? Badilikeni ili muondoe taswira mbaya mliyojenga kwa jamii, hatuwezi kuwa maadui kwa kuongea ukweli.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook