Your are here: Home // Habari // BARAFU AWAKUMBUKA KAJALA NA LULU

BARAFU AWAKUMBUKA KAJALA NA LULU

Suleiman Said

Barafu Mwigizaji na Mtayarishaji wa filamu Swahiliwood.

MWIGIZAJI na muongozaji wa filamu Swahiliwood Suleiman Said ‘Barafu’ yupo katika simanzi kufuatia wasanii walioshiriki katika filamu yake ya House Boy kusekwa ndani kwa makosa tofauti tofauti, wasanii hao ni Kajala Masanja na Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiongea na FC Barafu anasema kuwa katika filamu hiyo Kajala aliigiza kama mkewe na Lulu kama mwanaye.

Suleiman Said

Barafu akiwa Location na Script akipitia pitia.

.

“Kila nikiipitia filamu ya House Boy nawakumbuka sana wasanii wenzangu tulioigiza nao Kajala na Lulu ambao kwangu ni kama familia yangu kama nilivyoigiza nao katika filamu hiyo, hapa ndio unaona maisha ni ya ajabu mtu unaweza kupatwa na mikasa na kupotea katika jamii huku ikiwa bado jamii inakuhitaji kwa ajili ya kuwaelimisha na kuburudisha,”anasema Barafu.
.

Kajala Masanja, Wema Sepetu.

Kajala akiwa na Wema wakirekodi filamu ya House Boy.

Barafu anasema kuwa hata anapotaka kwenda kwa ajili ya kuwaona na kuwafariji anajikuta anakuwa katika wakati mgumu kwani tayari wasanii hawa tayari alikuwa amewaweka kama ni sehemu ya familia yake, kilichobaki kwake kwa sasa anawaombea kwa Mungu ili awape wepesi na matatizo yanayowakabiri, katika filamu hiyo wasanii walioshiriki ni Wema Sepetu, Kajala Masanja, Elizabeth Michael ‘Lulu’ Barafu na wasanii wengine.
.

Elizabeth Michael

Lulu msanii wa filamu akishikiliwa na Polisi katika Gereza la Segerea.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook