Your are here: Home // Habari // KANUMBA KUTUNIKIWA TUZO YA HESHIMA UBELGIJI (BELGIUM).

KANUMBA KUTUNIKIWA TUZO YA HESHIMA UBELGIJI (BELGIUM).

Steven Kanumba

Hayati Kanumba The Great enzi ya Uhai wake Swahiliwood.

Msanii nyota wa filamu Swahiliwood marehemu Steven Kanumba ataenziwa nchini BELGIUM ifikapo mwezi julay mwaka huu katika kilele cha sherehe za maadhimisho uhuru wa Burundi, katika maadhimisho hayo ambayo yatajumuisha wananchi wa nchi za Burundi ,Tanzania, Rwanda, Kenya, Congo DRC, Uganda wanaoishi ulaya pamoja na wageni toka nchi mbalimbali za Afrika na nchi za Ulaya watahudhuria katika tamasha hilo kubwa na la aina yake FC imeelezwa na waandaaji hao.

.

Steven Charles Kanumba

Kanumba The Great enzi zake akiwa katika pozi.

Wapenzi wa msanii Kanumba ‘The Great’ kutoka nchi zinazoongea lugha ya Kiswahili hususan Afrika Mashariki watapata fursa hiyo kumkumbuka marehemu Steven C. Kanumba kwa kutoa tuzo ya heshima kwa marehemu Steven Kanumba pamoja na kumuenzi kwa mchango wake mkubwa wa kupiga vita umasikini,kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili, kuleta umoja wa jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuelimisha pia kuburudisha watu wa jumuiya hiyo.

“Kwetu sisi Kanumba ni shujaa wa muungano tulionao, kwa sasa waafrika tunapokutana Ulaya tunahesabika kama familia moja, na tumekuwa tukitumia filamu kutoka Tanzania kwa ajili ya kujenga umoja wetu huku tukitumia Lugha ya Kiswahili kama kiungo chetu muhimu, kwa kuliona hilo sisi kama wakurugenzi wa Jami Burundi tumeandaa tuzo maalum kwa mpiganaji Steven C. Kanumba kwa mchango wake kupitia kazi zake za filamu, huku Ulaya Kanumba ni mtu mashuhuri sana,”anasema Chansard Mundele.
.

Kidumu Kibido

Kidumu mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza katika tamasha la kumuenzi Kanumba The Great.

Aidha tamasha hilo linaloandaliwa na asasi mashuhuri hapa Belgium JAMI BURUNDI chini ya rais wake bwana
CHANSARD MUNDELE pamoja na na mkurugenzi wa asasi ya JAMI BURUNDI Bwana Jumaine Ndayizeye ambao
wote ni raia wa nchini Burundi wametoa mwaliko kwa wasanii wa filamu wa kike wawili wa kitanzania ambao walikuwa wakifanya kazi na marehemu kwa karibu ambao watapokea tuzo hizo kwa niaba ya Watanzania wote kwa mchango wa bwana Steven Kanumba katika kuitangaza Afrika kwa lugha ya Kiswahili.
.

Nziza Desire

Nziza Desire naye atatumbuiza katika tamasha hilo la Kanumba Ubelgiji.

Pia Kampuni hiyo ya Jami Burundi imetoa mwaliko kwa wapenzi wa Kanumba waliopo ulaya yote kuudhuria sherehe hizo za Uhuru wa Burundi ambazo hufanyika kila mwaka na kipindi hiki kutapatikana fursa ya kumuenzi Hayati Steven Kanumba ambaye aliteka mashabiki katika jumuiya ya Afrika Mashariki.
.

Patcho Mwamba , Steven Kanumba

Patcho Mwamba na Kanumba The Great wakiwa sehemu ya kurekodi filamu, huyu pia alikuwa ni rafiki yake mkubwa.

Sherehe hizo zitapambwa na wasanii wa muziki kama Kidumu Kibido, Nziza Desire na wengine kibao michezo na burudani nyingi zitafanywa, aidha washiriki wa Miss East afrika Europe kama Cynthia Inkwene , na wageni toka nchi mbalimbali watahudhulia ,Mr. Chansard Mundele na Jumaine Ndayizeye wanapenda kuwakumbusha watu wa Afrika Mashariki kuwa na upendo na mshikamano na kutumia fursa hii kwa kumuenzi Nyota wa filamu Steven Charles Kanumba ambaye alisisitiza upendo na mshikamano kupitia kazi zake za filamu.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook