Your are here: Home // Habari // KOMEDI HAILIPI KAMA MUZIKI- SHARO MILIONEA.

KOMEDI HAILIPI KAMA MUZIKI- SHARO MILIONEA.

Hussein Mkiety

Sharomilionea Mchekeshaji Swahiliwood.

MCHEKESHAJI Mahiri katika tasnia ya uchekeshaji Swahiliwood Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’ amesema kuwa sanaa ya uchekeshaji kwake hailipi kama inavyolipa kwa wengine, kwani hadi leo bado hajaona fedha yake tofauti na muziki anaofanya, fedha nyinyi anapata kupitia muziki tofauti na kazi ambayo imemtambulisha yeye katika Ulimwengu wa sanaa ya uchekeshaji, lakini fedha kutoka katika muziki inaoneka kwa kupitia maonyesho mbalimbali anayoarikwa na kutumbuiza katika maonyesho hayo.

Hussein Mkiety

Sharomilionea akiwa katika pozi.

“Kwangu mimi sanaa ya uchekeshaji hailipi tofauti na muziki, kwa sasa nina single tatu tu lakini mafanikio yake nayaona kwa kupitia muziki pamoja nimekuwa ni maarufu kupitia uchekeshaji lakini malipo yanakuwa ni ya muda tu kwa sababu uigizaji kazi inakuwa siyo yako ni mali ya mtayarishaji kwa hiyo wewe unakuwa hauna chako tena,”anasema Sharomilionea.

Sharomilionea ambaye amekuwa maarufu kutokana na staili yake anayotumia katika kuigiza amesema kupitia muziki amefanikiwa kusafiri nje ya nchi na kufanya maonyesho na kulipwa vizuri, na bado anaendelea kupata miariko kwa ajili ya kufanya muziki pamoja na kuamini kuwa kuna baadhi ya wasanii wa kuchekesha ambao wamefaidika na uchekeshaji na kuweza kupata fedha kwa ajili ya kazi hiyo. Msanii huyo ambaye ana mkataba na Kampuni ya Al- Riyamy Production pamoja na kuigiza pia ni mwanamuziki wa kizazi kipya yaani muziki wa Bongo Fleva.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook