Your are here: Home // Habari // MSHINDO JUMANNE AACHANA NA SHARKS PRODUCTION.

MSHINDO JUMANNE AACHANA NA SHARKS PRODUCTION.

Mshindo Jumanne

Mshindo Jumanne Mtayarishaji na Muongozaji wa filamu Swahiliwood.

MSANII mwenye vipaji vingi katika tasnia ya filamu Swahiliwood Mshindo Jumanne ameachana na kampuni ya Sharks Production kampuni ambayo alikuwa ni meneja wake pia msanii huyo amedai kuwa kwa sasa hafikirii kufanya kazi katika kampuni nyingine baada ya kuona mara nyingine amekuwa anashindwa kuonyesha uwezo wake kiutendaji.

Mshindo Jumanne

Mshindo Jumanne akiwa katika pozi.

“Tasnia ya filamu kwa sasa inahitaji mabadiliko makubwa sana hasa katika usambazaji wa filamu kwa hiyo nilipokuwa na kampuni ya Sharks hilo ndilo lilikuwa ni wazo langu la kwanza katika kuleta mabadiliko lakini unakutana na upinzani kwa hiyo nifikiri ni bora kufanya kazi binafsi na kuimalisha kampuni yangu,”anasema Mshindo.
.

Mshindo Jumanne

Mshindo akiwa na mshiriki wa filamu mwenzake.

Mshindo ambaye ndiye msanii pekee mwenye vipaji vingi ana uwezo wa kupiga picha za video, kuhariri, kuongoza filamu na pamoja utayarishaji awali alikuwa na kampuni yake kwa ajili ya usambazaji na utayarishaji wa filamu iliyojulikana kwa jina SSG Distributors kwa anasema kampuni yake imetayarisha filamu mpya zaidi ya tatu ambazo anatarajia kuanza kusambaza kupitia kampuni yake kuanzia sasa na yupo safarini Zanzibar kikazi akirudi kila kitu kitakuwa sawa.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook