Your are here: Home // Habari // NATASHA NI KIUNGO MUHIMU SWAHILIWOOD.

NATASHA NI KIUNGO MUHIMU SWAHILIWOOD.

Susan Lewis

Natasha Msanii kiungo muhimu Swahiliwood

MWIGIZAJI na mwandishi wa muswada Swahiliwood Susan Lewis ‘Natasha’ ndiyo msanii pekee mwenye mawasiliano na wasanii wote bila kujali itikadi au kundi lolote uchunguzi wa FC umegundua na kumtangaza kama ni kiungo muhimu katika mawasiliano kwa wasanii na wadau wa filamu Swahiliwood anastahili pongezi Mama Bora.

Susan Lewis

Natasha akiwa katika moja ya Sherehe za wasanii.

Kufuatia siku ya akina mama kufanyika mwezi huu basi ni wakati wa kutambua na kumtambua kuwa ni mama bora na mlezi wa tasnia hiyo ya filamu hapa nyumbani, Natasha anastahili sifa hiyo kwa sababu moja kuu kuweza kuwasiliana na kila msanii, mdau wa tasani ya filamu pale inapotokea taarifa yoyote iwe sherehe hata misiba.

Natasha ni mtu ambaye amejitoa kwa kila hali kuhakikisha kuwa inapohitajika taarifa iwafikie wasanii akiipata taarifa utuma ujumbe wa simu kwa kila mdau na wasanii kwa ujumla wake na kuhudhuria pia, kwa mantiki hiyo tunaona kuwa anastahili kutangazwa kama mshindi wa Amani kwa mwaka 2011 na 2012 Natasha akiwa pia kama mwanahabari amekuwa akitumia nafasi yake vema kwa kuwafikishia ujumbe wahusika kwa wakati.

Jambo la kujivuni kwa msanii huyu ni pale alipoweza kuepuka makundi ambayo kwa sasa ni tatizo ukiongea na Natasha yeye hajui kuhusu TAFF wa la Bongo Movie Unity bali yeye anaamini kuhusu upendo wa kila msanii na wadau wote kwa ujumla, kwa moyo huo anastahili kuitwa Mama bora na mtoa taarifa mahiri anayeweza kuunganisha jamii.

Susan Lewis

Natasha akiwa naye ushiriki msosi pia....

Pengine kwangu mimi naamini kuwa iwapo Natasha akipewa dhamana ya kuwaongoza wasanii makundi yote yatavunjika na kuwa na umoja wa kweli usio na shaka, tunamhitaji mtu kama Natasha kuwa kiongozi najua wazi kuwa hakuna msanii mwingine anayeweza kutuma ujumbe kwa ajili ya tatizo au taarifa kwa wasanii na wadau wote, kwa sababu kila ujumbe ukitumwa ni fedha inahitaji moyo kama wa Natasha.

Pia nampongeza kwa malezi bora kwa mwanaye Monalisa kwani naye ni msanii anayejiheshimu hana makundi na ni mtu wa kazi, basi wakati wenzetu wiki hii walikuwa wakisherekea siku ya mama basi nasi tunashererkea siku hiyo kwa kumtambua Natasha kama Mama Bora na mlezi mwema Swahiliwood asante kwa moyo wako Mungu akupe nguvu na uhai mrefu uongoze tasnia ya filamu Swahiliwood.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook