Your are here: Home // Habari // AROBAINI YA BI. CHAIBA KOMBO KUFANYIKA JUMAPILI HII.

AROBAINI YA BI. CHAIBA KOMBO KUFANYIKA JUMAPILI HII.

Bi. Chaiba Kombo

Bi. Chaiba Kombo Mwanaharakati na mwandishi wa muswada Swahiliwood.

FAMILIA ya Mwanaharakati na mwandishi mahiri wa muswada wa filamu Swahiliwood Bi Chaiba Kombo inawakaribisha jamaa ndugu wadau wote wa tasnia ya filamu katika Arobaini ya kumaliza msiba wa ndugu yao siku ya jumapili tarehe 27. May. 2012, shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika Kimara Kona kwa Mzee Masabo.

Tukio hilo linatarajia kuanza kuanzia saa mbili asubuhi , Bi. Chaiba Kombo alifariki tarehe 22. April. 2012 na kuzikwa Kimara mwanadada huyo alikuwa ni mwanaharakati na mtafiti wa mambo yake kale pia mwandishi wa makala za mambo ya kale makala ambazo alikuwa akiziandikia katika vyombo vya habari mbalimbali hapa nyumbani na nje ya nchi.

Bi. Chaiba Kombo

Bi. Chaiba Kombo enzi za Uhai wake.

Pia Bi. Chaiba Kombo alikuwa akiandika michezo mifupi mifupi na kurekodi ambayo aliipa jina la ( Hekaya za Wakubhubha ) ikimananisha Mfululizo wa Hadithi zisizosimuliwa za Tanzania na kati ya michezo hiyo ilirushwa kupitia Televisheni ya Channel Ten huku akiandikia makala za utafiti kuhusu mtu wa kwanza (Zinjanthropus) ambaye inasemekana alipatikana , Ziwa Olduvai Gorge Tanganyika mwaka 1959.

Karibu tumuenzi mwanaharakati Bi. Chaiba Athuman Kombo siku hiyo ya jumapili na kuendeleza kazi zake , usikose makala maalum ya mwanaharakati huyu kupitia hapa hapa FC.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook