Your are here: Home // Habari // MZEE SMALL ALAZWA AMANA HOSP.

MZEE SMALL ALAZWA AMANA HOSP.

Said Wangamba

Mzee Small mwigizaji wa filamu na vichekesho Swahiliwood aliyelazwa Hospitali ya Amana,

GWIJI la Sanaa na mwigizaji filamu na vichekesho Swahiliwood Said Wangamba ‘Mzee Small’ amelazwa katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam Mzee Small alilazwa katika Hospitali hiyo baada ya kuugua ghafla akitokea safarini Jijini Mwanza alikokwenda kwa ajili ya kuelimisha kupitia sanaa kukomesha mauaji watu wenye matatizo ya ngozi Albino.

Said Wangamba

Mzee Small akiwana mwigizaji mwenzake Bi. Chau.

“Ameanza kuumwa tu baada ya kurudi Mwanza tatizo kubwa ni Pressure ambayo imemsabishia ugonjwa huu ambao imekuwa kama ghafla kwa sababu hakuwana na dalili za ugonjwa kama huu wa kiharusi,”anasema rafiki yake Seif Mbembe.

Aidha wauguzi wa Hospitali hiyo walijikuta wakiingia matatani baada ya kutofautiana na mtoto wa Mzee Small wa kike kutokana na ucheleweshaji wa huduma kwa mgonjwa, katika safari ya Mwanza aliambatana na Mwigizaji mwenzake Chausiku Salum ‘Bi. Chau’, wasanii mbalimbali wamejitokeza katika Hospitali hiyo kwa ajili ya kwenda kumfariji msanii mwenzao, pia wadau wanaombwa kumuombea msanii huyu ili arudi katika afya yake awali.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook