Your are here: Home // Uchambuzi // Filamu ya Apple iliyoenda mbele kuliko wakati uliopo

Filamu ya Apple iliyoenda mbele kuliko wakati uliopo

apple. film c

Filamu ya Apple ya kitanzania.

KATIKA uchambuzi wetu leo tunaichambua filamu ya Apple iliyoandaliwa na mwanadada Irene Uwoya na kuwashirikisha wasanii nyota wanaotamba kwenye tasnia ya filamu Bongo, moja ya changamoto katika filamu hiyo ni hadithi iliyotungwa na Irene Uwoya na kuandikwa na Ali Yakuti.
Filamu hiyo imeongozwa na Single Mtambalike, mwigizaji mkongwe katika filamu Bongo, hadithi yake kwa ufupi ni kwamba tunda la Apple linavuruga uhusiano wa Baba Haji na Irene Uwoya baada ya Irene kuchukua tunda hilo katika friji na kuondoka nalo.

Irene Uwoya

Irene Uwoya Mwigizaji wa filamu Swahiliwood.

Baba Haji anaamka na kubaini kuwa halipo, anaamua kumtafuta mkewe ambaye ndiye kaondoka nalo, hapo ndiyo mwanzo wa filamu, nimekusimulia kwa ufupi ili uende ukaitafaute na kuiangalia kwa umakini, hadithi ni tata kwa sababu Tanzania hatuna mashirika binafsi ya kipelelezi.

Hadithi: Mtunzi wa hadithi hii hakufanya utafiti kuhusu hali halisi ya Mtanzania na Afrika kwa ujumla wake, tunamuona Irene akitafutwa kama muuaji, lakini picha inamuonyesha moja kwa moja kama hausiki, hapa mwandishi hakuonyesha (Conflict ) kisa mkasa, na kufanya hadithi kuyumba.

USAILI: Mtu wa usaili (Casting Director) alifanikiwa kuchagua watu ambao waliweza kumudu sehemu zao, japo kuna baadhi ya wasanii waliwekwa kulingana na soko linavyosema, iwe hivyo kwa maamuzi ya wanunuzi wa kazi hizo.
MAVAZI: Mtu wa mavazi (Costumes Director) alifanikiwa kuwavalisha wasanii, anastahili pongezi, wasanii walipendeza na kuonekana.

MAPAMBO: (Makeup) Mtu wa mapambo yupo sawa, aliweza kuwatengeneza vizuri wasanii na kuonekana vizuri hasa sehemu ambayo kichaa alicheza, alicheza vema na kuonekana kichaa kweli.
MANDHARI: Mtu wa mandhari (Location manager) alifanikiwa sana katika kutafuta sehemu za kurekodi, zilistahili kulingana na matukio yaliyoonyeshwa katika filamu hiyo, anastahili pongezi.
MWANGA: Mtu wa mwanga (Lights man) alifanikiwa katika kupanga taa na kufanikiwa kuweka mwanga sahihi na kumwalika vema katika matukio husika, anastahili pongezi zake.
.

Apple film

Filamu ya Apple iliyochambuliwa

Irene Uwoya

Irene Uwoya mwigizaji wa filamu Swahilihood

SAUTI: Mtu wa sauti (Soundman) alikuwa poa, sauti katika filamu hii imesikika vizuri na kumfanya mtazamaji asiwe na usumbufu wa kupandisha sauti na kushusha mara kwa mara.
MHARIRI: Mhariri alifanya kazi yake vema, ndiyo maana hatuoni makosa yakijitokeza na kuwa mengi kwa kiwango cha juu katika kutengeneza filamu nyingi ambazo hutengenezwa kwa bajeti ya chini.

MUONGOZAJI: Muongozaji (Director)ni mtu muhimu sana katika kuhakikisha filamu inakuwa bora kulingana na hadithi husika kwa kulinda wazo la mwandishi au mtunzi, ukiangalia filamu hii unaweza kubaini kuwa hakukuwa na mtiririko uliofuata hadithi husika, kama kawaida filamu ikifanya vizuri sifa zinaenda kwa muongozaji lakini kwa hii hapana.

Filamu ya Apple, mtunzi alitumia teknolojia ya juu, lakini hakuna utafiti uliofanyika, kwani ukiangalia memory card iliyokuwa inatafutwa haikupatikana hadi mwisho wa filamu na kuonekana kama ni kulazimisha matukio ya siri, visa vya kulazimisha.

Bongo hatujafikia kuwa na mashiriki binafsi ya kijasusi, nimeangalia hadi mwisho sikupata jibu la filamu husika na kujikuta nina maswali mengi yasiyo na majibu, ni kazi inayoonekana kutumia gharama kubwa lakini haiendani na matunda ya filamu husika, utafiti ni jambo la muhimu sana.

filed under: Uchambuzi

1 response to "Filamu ya Apple iliyoenda mbele kuliko wakati uliopo"

  1. nasser says:

    Kwenye Film hakuna mtu anayeitwa (Costumes Director)
    Kuna Costumes designer.

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook