Your are here: Home // Uchambuzi // USAMBAZAJI MBOVU WA FILAMU BONGO

USAMBAZAJI MBOVU WA FILAMU BONGO

Filamu ya Ungo

Ungo moja ya filamu Swahiliwood.

Tasnia ya filamu kwa Tanzania kila siku uzalishaji unazidi kuchukua kasi, huku watengenezaji wa filamu wakijitahidi kuibuka na vifaa vipya kila siku, lakini jambo moja tu ambalo limeshindika au hakuna mtu ambaye ameliona na kulifanyia kazi ni utafutaji wa Masoko na matangazo(Marketing and Promotion).

Hukumu ya ndoa yangu

Filamu ya JB Hukumu ya Ndoa yangu

Yvonne Cherryl, Wastara Juma, Issa Mussa

Wasanii wa filamu wakiwa nchini Uingereza

Filamu ya Ungo

filamu ya Ungo

Umahiri umekuwa katika utengenezaji huku suala la mauzo na utangazaji zikiachwa bila kutafutiwa ufumbuzi, mfumo ulikuwepo wa usambazaji wa filamu ni mbovu sana, hautoi fursa ya kukusanya fedha na kuweka mgawanyiko sahihi kwa wahusika wa filamu na kuibuka malalamiko kila uchwao.

Kuna hatua ambazo mara nyingi hufuatwa na wasambazaji wa filamu sehemu kama Hollywood, Bollywood, lazima msambazaji baada ya kukabidhiwa filamu husika jambao la kwanza kwao ni kuingia katika Promotion huku wakifuatilia suala la masoko ambayo yatawapa uhakika wa soko.

Mara nyingi wasambazaji (Distributors) ujipanga kwa kufanya matangazo kwa muda mrefu huku wakiwa tayari kwa ajili ya kuwaweka tayari wapenzi wa filamu kwa ajili ya kuliandaa soko, matangazo haya moja kwa moja ufanyika sehemu husika ya biashara hiyo katika majumba ya sinema.

Filamu matangazo yake yanakuwa katika hatua nyingi lakini kuu ni Teaser, Trailer na Behind the Scene, lakini hayo ni matangazo ya moja kwa moja katika majumba ya sinema, matangazo mengine ni katika Televisheni, Radio na Majarida ya filamu na hata yale yasiyo ya filamu kwa maana magazeti mahiri ya habari.

Baada ya msambazaji kujiridhisha na kupokea oda za kutosha uingiza sinema yake sokoni, tena fedha taslimu kwani wana mikataba na majumba ya sinema Duniani, lakini hapa kwetu hali ipoje?

Swahiliwood hali si shwari, kwani awali walioanza kufanya kazi ya filamu walianza vema kwa filamu zao kuonyeshwa katika majumba ya sinema, filamu ya Shamba kubwa, Augu, Love Story Tanganyika na Unguja na nyinginezo zilionyeshwa katika majumba ya sinema tena karibu nchi nzima.
.

Filamu ya F.B.I

Filamu ya FBI ya SeBa

Kigodoro film

Filamu ya Kigodoro Kanitangaze inayosumbua sokoni

Kufuatia mlipuko wa filamu kushamiri nchini, mwaka 2003/2004 utaraitibu huo ulibadilika na kuanza kuuza filamu katika Dvd, Vhs, Vcd badala ya kuendelea katika utaratibu uliozoeleka wa kuonyeshwa katika majumba ya filamu hapo ndipo makosa ya awali yalipofanyika na kuliacha soko bovu.

Leo kila msambazaji akija lazima akimbie katika soko lilojaa maharamia kutokana na kuwa na mfumo usiokubalika dunia katika usambazaji wa filamu kwani katika biashara zilizo na fedha ya moja kwa moja ni sinema kwani ina vyanzo vingi vya mauzo.

Kazi zetu zinategemea muuza katika Dvd tu, biashara isiyo na uhakika lakini kama tungeweza kutumia mifumo ya wenzetu kama vile kufanya matangazo kwa ajili ya filamu, jambo linguine ambalo kwetu tumesindwa kufanya ni kuuza filamu kwanza katika majumba ya sinema.

Kuzalishalisha vitu vingine kama katuni, michezo, wasifu jina mauzo mengine, kwa hapa inawezekani ni kutokana na uhaba wa teknorojia na ujuzi wa ufanisi wa vitu hivyo basi, wasambazaji wabaki katika kutengeneza sinema zenye sifa ya kuingia katika majumba ya sinema.

filed under: Uchambuzi

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook