Your are here: Home // Habari,Uchambuzi // WASANII BONGO TUMIENI FURSA YA ZIFF KUJIFUNZA

WASANII BONGO TUMIENI FURSA YA ZIFF KUJIFUNZA

Prof. Martin Mhando

Mkurugenzi wa ZIFF Prof. Martin Mhando akiwa na mdhamini wa Zuku

Tamasha kubwa la filamu nchi za Majahazi Zanzibar Internation Film Festival (ZIFF), katika kuazimisha tamasha la 17 ambalo linatarajia kufanyika tarehe 14 June 2014, Zanzibar ni tamasha ambalo limezidi kupata mafanikio kwa kuwa kiungo cha wadau wa filamu Ulimwenguni.

.

Daniel Nyalusi

Dan Nyalusi meneja wa Tamasha ZIFF

Husna Sajenti

Wadau wa filamu wakimsikiliza Prof. Mahando hayupo pichani.

Jacob Stephen

Jb akisikiliza kwa makini ujio wa tamasha la ZIFF

Suleiman Barafu, Daud Michael

Wasanii Barafu na Duma walikuwepoa pia

Simon Mwakifwamba, Stevene Mangere

Mwakifwamba Rais Taff na Steve Nyerere Mwenyekiti Bongo Movie walikuwaepo

Moja ya sifa ambayo mkurugenzi Profesa Martin Mhando wa Tamasha hilo anajivunia ni kuweza kupokea zaidi ya filamu 79 ambazo zitaonyeshwa katika tamasha hilo kwa siku 10, filamu za kiafrika ukanda wa nchi za Mahajazi, filamu zimepokelewa kutoka nchi 35, kukiwa na filamu fupi 38, filamu 23 na makala (Documentaries) 18.

Tamasha hili ambalo lilianzishwa mwaka 1997 limekuwa ni kiungo kikubwa cha wadau wa tasnia ya filamu, watengenezaji wa filamu, na wanafunzi wanaojifunza kutengeneza filamu, pia tamasha hili limefungua njia kwa uwepo wa East and Central African Film.

Zanzibar International Film Festival (ZIFF) tamasha la 17, ambalo mara nyingi hufanyika katika maeneo ya Stonetown huku mchangiaji mkuu akiwa ni UNESCO wakitaka kulinda na kutangaza hifadhi za kitalii zilizopo Stonetown.
Moja ya faida kubwa kwa wasanii na watengenezaji wa filamu kwani ZIFF imeandaa semina ya siku 10 kwa wadau wa filamu itakayoendeshwa na Maisha Lab kozi ambayo itaendeshwa kwa Lugha ya Kiswahili na kutoa fursa kwa wahusika kufahamu vema.

Katika kuhamasisha mkurugenzi wa Maisha Lab Mr. Fibby Kioria ametoa ofa kwa washiriki 15 ambao watalipiwa gharama za maradhi na chakula wakiwa Zanzibar wakati wa kozi hiyo ambayo itakuwa ni ya Uandishi wa Muswada kwa muda wa siku 8.
Kufuatia ushiriki wa filamu za Swahiliwood kuwa ushiriki wake ni mdogo, ndio maana tunasema kuwa wasanii wetu ambao ndio watengenezaji wa filamu hapa kutumia fursa hiyo katika kujifunza jinsi ya kusoma uandishi bora wa mswada wa filamu.

Ni imani yetu kuwa endapo wasanii wetu wataweza kupata elimu kupitia walimu waliobobea na kujifunza lazima tasnia ya filamu itakuwa na kutoa mwanya kwa wasanii kushiriki katika matamasha makubwa ya filamu ikiwepo ZIFF, ni wasaa mzuri katika kujifunza.

Historia inaonyesha kuwa katika suala la kujifunza lipo nyuma sana kwa wasanii wetu ambao ndio watayarishaji na waandishi wakuu wa miswada ya filamu wanazoshiriki katika uigizaji, wasanii wengi wanafanya kazi kwa kipaji na si weledi wa fani hiyo
.

Rashid Mrutu, Anael Kiule, Zuber Mohamed

Mrutu, Anael na Niva wakiwa katika mkutano wa Ziff

Prof. Martin Mhando

Prof. Mhando akiwa katika mkutano na wadau wa tamasha la ziff.

Prof. Martin Mhando

Prof. Mhando akionyesha muonekano wa ZIFF mwaka huu

Pia mratibu wa tamasha hilo Daniel Nyalusi alitoa somo kwa watayarishaji wa filamu kuwa makini na utayarishaji wa sinema kwani endapo haiwezekani kutengeneza filamu moja tu kwa ajili ya kushiriki ni vema wakatenganisha kuwa na filamu maalum kwa ajili ya kushiriki katika matamasha ya filamu.

Filamu zetu nyingi zinagawiwa vipende viwili na kupewa jina la part 1 na 2, ugawaji wa filamu kwa aina hiyo haupo inawezekana ndio moja ya sababu ya filamu zetu kutoshiriki katika matamasha ya ndani na nje pia, ambayo pamoja ushiriki wa filamu za Bongo movie ni mdogo sana.

Hivyo kutokana na uoga wa watengenezaji wetu filamu zetu zimebaki kushindana katika kipengele kimoja tu cha Zuku Bongo Movie Swahili ni usiku maalum hufanyika kwa ajili ya kuonyesha na kutoa tuzo kwa wasanii waliofanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo.

filed under: Habari,Uchambuzi

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook