Your are here: Home // Habari // UNATAKA KUWA NYOTA WA TAMTHILIA NA FILAMU?!

UNATAKA KUWA NYOTA WA TAMTHILIA NA FILAMU?!

Mshindo Jumanne

SuperDirector Mshindo Muongozaji wa filamu Swahilihood

KAMPUNI maarufu ya filamu Swahilihood ya Safina Movies imeandaa nafasi za bure kabisa kwa msanii yoyote mwenye kipaji kujiunga na kampuni hiyo kwa ajili ya kuonyesha kipaji chake, msanii chipukizi atakayejiunga na kundi hilo atafundishwa na kushiriki katika kazi za kampuni hiyo.

Mshindo Jumanne

Mshindo akiwa katulia katika pozi.

Mshindo Jumanne

Director Mshindo akiwa katika pozi.

Akiongea na wanahabari mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Mshindo Jumanne amesema kuwa kampuni hiyo imekusudia kukuza vipaji vya wasanii chipukizi waliokosa fursa hiyo pamoja na kuwa na uwezo wa kuigiza kwa vitendo na si maneno.

“Wasanii wenye vipaji ni wengi sana mitaani lakini hawapewi fursa kuigiza na kushiriki katika filamu na tamthilia, ndio maana kampuni yetu ya Safina Movies imeliona hilo na kuwapa nafasi za kuonyesha vipaji vyao bila gharama,”anasema Mshindo.

Mkurugenzi huyo amedai kuwa kutokana na ugumu wa ajira nchini Tanzania baadhi ya wasanii chipukizi wamejikuta wakitapeliwa kwa kuchangishwa fedha na kuuziwa fomu kwa gharama kubwa na kuishia kupigwa picha bila kupewa kazi.

Aidha kampuni ya Safina Movie yenye maskani yake Kijichi Mbagala inasajili wanaohitaji kuwa wasanii nyota Bure kabisa kama msanii anahitaji anaweza kuwasiliana na uongozi kwa namba hizi 0658 010 100/ 0752 132 347 utakuwa umeingia katika tasnia ya filamu.

Safina movie inahitaji wasanii zaidi ya 400 kwa ajili ya tamthilia inatayorushwa katika moja ya televisheni kubwa za Afrika Mashariki, kampuni hiyo ambayo ni watengenezaji na wasambazaji wa filamu nchini imesema pia wasanii hao pia watashiriki katika filamu za kampuni hiyo.

filed under: Habari

3 responses to "UNATAKA KUWA NYOTA WA TAMTHILIA NA FILAMU?!"

  1. Helo..,nimependa kazi zenu za sanaa,na mm ningepena nijiunge ktk kampuni yenu..kwa sababu ninakipaji cha kuigiza,na ninatumain nitafanya vzr.

  2. HASSAN MOHAMED(BIKO) says:

    naitwa hassan mohamed nimepata taarifa zenu za kuibua vipaji nami natamani kuwa mmoja wapo kati vijana watakao shiliki ktk hiyo project asante kazi njema

  3. Mm naitwa jackson leopord in mwanafunzi naye malza masomo yangu ya kidato cha sita no muigizaji, dancer NA naweza kuandika tamthilia za kusisimua. Naomba kuwa chini yenu Muone kipaji changu

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook