Your are here: Home // Uchambuzi // THAMANI YA MSANII NI KULIPWA FEDHA NYINGI AU KUIGIZA SCENE NYINGI?

THAMANI YA MSANII NI KULIPWA FEDHA NYINGI AU KUIGIZA SCENE NYINGI?

Van Vicker

Van Vicker mwigizaji kutoka Ghana

UNAPOKUWA Bongo hasa katika tasnia ya filamu kuna mambo ambayo unaweza kukutana nayo na kichwa kikataka kupasuka, kuna mifumo iliyopo hakuna kokote Ulimwenguni ufuatwa na wasanii wa filamu katika malipo, ni pale msanii anaposhindwa kutambua thamani yake katika malipo.

Irene Uwoya

Mwigizaji wa kike Irene Uwoya

Blandina Chagula

Johari mwigizaji wa kike mkongwe

Van Vicker

Van Vicker akiwa na Monica katika scene

Van Vicker

Van Vicker katika pozi

Van Vicker Wellu sengo

Van Vicker akiwa Welu

Mara nyingi wasanii wamekuwa wakitaka wanaposhirikishwa katika filamu za watu ni kupangwa sehemu yote ya sinema hata kama hana uhusika wa filamu hiyo, na wapo tayari kulipwa fedha kidogo ili mradi tu, washiriki katika scene zote, tabia hizo zipo kwa wasanii wakongwe.

Lakini pamoja na kushiriki filamu na wasanii wenye majina kutoka nje hajiringanishi na kutambua thamani yao, mfano mzuri alipokuja msanii kutoka Ghana Van Vicker iliripotiwa kuwa msanii huyo alicheza scene 10 tu kwa dola 10,000 mbona hakusema anataka kucheza sinema nzima?

Swali linakuja je thamani ya msanii ni kulipwa fedha nyingi au kuigiza scene nyingi? Ni jambo la kuchekesha kama si kushangaza, mtu anatakiwa alipwe kwa kushiriki scene labda lakini tatu lakini anakataa kwa kuamini kuwa kuigiza sinema nzima ndio ataonekana.

Baada ya mapatano kushindikana kutokana na masharti yake anakubali kwa shingo upande kuigiza scene moja aliyochaguliwa lakini akitaka alipwe milioni moja na nusu ambayo alitaka alipwe kwa kucheza sinema nzima hapo tunajiuliza je inatakiwa fedha au kuonekana sana?

Wasanii wengi wa Swahilihood wanaonekana ni watu wa kubahatisha hivyo wana hofu kuwa endapo atapatiwa sehemu ndogo huwezekano wa kuonekana na kuvutia watazamaji atakosa kwani baadhi yao hawajiamini wanajua kuwa wanahitaji kupewa scene nyingi kuliko hata fedha.

Thamani ya msanii inajengwa kwa kulipwa vizuri pasipokujali kuwa ameshiriki kuigiza katika scene nyingi na malipo yake yakawa pale pale, lakini inasemekana kuwa wasanii baadhi yao upenda kulipwa pengine hata hawataki malipo kwani kuna biashara zao.

Biashara hizi zisizo rasmi huhitaji msanii kuwa na filamu nyingi tu akiuza sura na hatimaye kuhesabu uwingi wake kama alama ya yeye kufanikisha mambo yake pasipo kujenga thamani yake ambayo itamfanya asiishi kwa mizinga au kubahatisha.

Tunashauri wasanii kujikita katika kutafuta thamani yao na si kuuza sura kwani hadi hakuna msanii anayejua thamani yake katika uigizaji anastahili kulipwa kiasi gani cha fedha anaposhiriki sinema japo kwa scene chache.

filed under: Uchambuzi

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook