Your are here: Home // Habari // BRAYANCE WORKS PRODUCTION KUKUPA DILI

BRAYANCE WORKS PRODUCTION KUKUPA DILI

Brayance orks

Kampuni ya Brayance Works

KAMPUNI ya Brayance Works Productions ya jijini Dar es Salaam inatarajia kuandaa kozi maalum kwa watengenezaji wa filamu na Video za muziki wa injili na makala za Video kwa ujumla, akiongea na FC mkurugenzi wa kampuni hiyo amesema kuwa wameamua kujenga tasnia katika Weledi.

Hassan Mbangwa

Mbangwa mkurugezi Brayance Works akiwa pozi.

Brayance Works

Kampuni ya Brayance Works waandaaji wa semeni ya Video

“Kampuni yetu imekusudia kutoa elimu kwa wadau wa tasnia ya filamu na Muziki wa Gospel na kazi zote za Video , huku lengo kuu ikiwa ni kuingia katika ushindani wa kibiashara na kimataifa, hivyo ni nafasi kwa wadau kutumia fursa hii adimu kutokea,”anasema Mbangwa.

Kozi hiyo itaanza rasmi tarehe 14/12/2015 hadi 19/12/2015 itafanyika katika Hoteli ya Green Light Tabata Shule, muda kuanzia saa 9 hadi saa 12 na 14 hadi 17 ada ni 125,000/ tu kwa mshiriki mmoja.

Sifa za washiriki kuanzia kiwango cha elimu ya Form 4-6 vyuo na pia kwa watayarishaji wa filamu na muziki wanaruhusiwa kushiriki katika kujikuza zaidi na kukamata masoko ya kimataifa.

Mada zitakazo fundishwa ni Matumizi sahihi ya Kamera (Camera works & setup), Mbinu za kusimamia Video (Directing Management & Techniques), Uwekaji wa rangi na kanuni za uhariri Video (Editing Principles & color balance), Uandaaji na upangaji wa Taa ( outdoor & Indoor Light setup), Uandaaji na utafiti wa Mandhari (Location Management).

Ni fursa ya kipekee kabisa kutokea weka ahadi kuwa hautakosa nafasi adimu kutokea nchini Tanzania walimu waliobobea katika masuala ya utengenezaji filamu na Video Afrika Mashariki watakuwezesha kuwa wa kimataifa. kwa mawasilino ni 0717 936 148 na 0754 762 613. Nyote Mnakaribishwa.

filed under: Habari

1 response to "BRAYANCE WORKS PRODUCTION KUKUPA DILI"

  1. Dir
    Mbangwa Hassan mimi ni mwanafunzi ninaejifunza mambo mbalimbali yanayo husiana na video prodaction.Naomba msaada wako kwani nimevutiwa na kazi zako nilikua na omba kufahamu kuhusu camera uliotumia kwenye video ya rose muhando hasa kwenye wimbo wa MUNGU UNASHANGAZA.

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook