Your are here: Home // Habari // NILIUZA KILA KITU NINUNUE SMART PHONE NIWASILIANE NA MASTAA – JITU

NILIUZA KILA KITU NINUNUE SMART PHONE NIWASILIANE NA MASTAA – JITU

Hassan Daffur

Jitu mwigizaji chipukizi Sahilihood.

TUPO mwezi wa tano kwa mwaka 2016 kwangu mimi kama utanitokea na kuniuliza msanii wako wa miezi mienne bora ni nani? Basi bila hofu wala kupepesa macho nitakujibu tu ni kijana mahiri katika kuigiza naye si mwingine ni Hassan Daffur ‘Jitu’.

Hassan Daffur

Jitu kijana hatari katika tasnia.

Hassan Daffur

Jitu katika muonekano nje ya scene.

Hassan Daffur

Jitu kazini

Hassan Daffur

Jitu akikamua ndani ya scene zake ukikutana naye utampenda.

Hassan Daffur

Jitu katika moja ya scene akikamua katika filamu ya Mhuni.

Hassan Daffur

Jitu akiwa katika pozi la picha kazni.

Naongea na kijana huyo mpole mtulivu mwenye nidhamu adimu kuipata kwa wasanii wetu wa Bongo Movie hasa pale wanapokuwa na uhakika wa kupata scene za kutosha kwa kila sinema, ananipa jibu moja si rahisi kulikamata game Swahilihood.

Jitu anasema kuwa zaidi ya miaka mitatu alikuwa anamtafuta mtu wa kumsapoti aweze kuonyesha kipaji chake kama ni muigizaji mwenye viwango vikubwa lakini hana sehemu ya kuonyeshea, hivyo aliwaza njia rahisi ni kununua simu smart phone.

“Nilinunua smart phone nikiamini kila msanii hakosekani katika social network hivyo kazi yangu nikutafuta akaunti zao na kuwatumia maombi, lakini majibu yalikuwa ya kukatishana tamaa,”

“Nikafunga na kuomba hadi nilipokutana naDirector Tico na kunifanyia interview na kunikubali, nikiwa na machungu na kumshukru Mungu nilijiapizia kufanya vizuri na ikawa hivyo,”anasema Jitu.

Jitu amekuwa kivutio hata kwa wenzake kwani ni msanii mwenye muonekano tofauti uhalisia wa maisha yake halisi ni mpole lakini ukimpatia nafasi ya vijana watukutu utafurahi kazi yake, anafanya kazi kulingana na uhusika wake.
Katika filamu ya Mhuni amefanya mambo makubwa sana ambayo huweza kuamini hata uone huyu ndio Jitu kijana mwenye muonekano wa kipekee na anayejali kazi yake akiwa na matumaini kuwa wa kimataifa.

filed under: Habari

2 responses to "NILIUZA KILA KITU NINUNUE SMART PHONE NIWASILIANE NA MASTAA – JITU"

  1. n says:

    Nidhamu na kazi nzuri inafanya sote tumuamini matumainii yangu atafika mbali sanaaa

  2. Nidhamu na kazi nzuri inafanya sote tumuamini matumainii yangu atafika mbali sanaaa
    Toka niingiee timamu nimemuona nidhamu yakee na kazi yakee kwa ujumla

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook