Your are here: Home // Uchambuzi // ASANTE TIMAMU KWA KUNIAMINI- JITU

ASANTE TIMAMU KWA KUNIAMINI- JITU

Hassan Daffur

Jitu mwigizaji wa filamu kutoka Swahilihood.

MWIGIZAJI chipukizi anayetishia nafasi za wasanii nyota wenye aina ya uigizaji wa kibabe Hassan Daffur ‘Jitu’ amefunguka kwa kusema kuwa kufika hapo alipo haikuwa rahisi kwani aliuza vitu vingi sana ili kuwasiliana na wasanii wakubwa lakini alikosa nafasi ya kuonyesha kipaji chake.

Hassan Daffur

Jitu mwigizaji anayetishia nafasi za wasanii wakongwe Bongo.

Hassan Daffur

Jitu katika pozi la picha

“Nilikuwa najua kama mimi ni mkali lakini nawezaje kuonyesha kipaji changu bila kupata nafasi nilitafuta smart phone kuwatafuta wasanii wakubwa sikujibiwa hadi siku moja nilipowasiliana na Tico akiwa Marekani na kunisaidia,”anasema Jitu.

“Nashukru kwa Director Tico kuniona kuniamini na kunipa nafasi katika kampuni ya Timamu African Media kuweza kushiriki kazi zake naona fahari,”anasema Jitu.

Msanii huyu Jitu kwa muda mfupi ameonyesha mafanikio makubwa katika uigizaji na kutishia nafasi za baadhi ya wasanii wenye muonekano kama wake hasa zile sinema za kibabe na kipaji chake kimeibuliwa na Timamu African Media baada ya kushinda katika usahili alioshiriki siku za nyuma.

filed under: Uchambuzi

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook