Your are here: Home // Habari // WASANII WAKONGWE WAMETUHARIBIA- SHIFFER

WASANII WAKONGWE WAMETUHARIBIA- SHIFFER

Sharifa Mansoor

Shiffer Mwigizaji wa filamu Swahilihood

MWIGIZAJI chipukizi kutoka tamthilia ya Siri za familia Sharifa Mansoor ‘Shiffer’ amesema kuwa uigizaji ni kazi sawa na kazi nyingine lakini walioanza walitumia fursa yao vibaya kwa kufanya mambo yasiyofaa kujikita katika masuala ya kashifa kitu kilichopelekea jamii kudharau fani hiyo.

Sharifa Mansoor

shiffer mwigizaji wa filamu Swahilihood

Sharifa Mansoor

Shiffer mwigizaji wa tamthilia ya Sir za Familia

“Haikuwa rahisi nilipoomba familia yangu kujiunga na Siri za familia kila mtu alisema kuwa naenda kupotea lakini nilijieleza na kukubaliwa sasa wananielewa nafanya kazi, shida waliotangulia walituharibia,”alisema.

Shiffer anasema kuwa wasanii waliotangulia walijisahau na kushindwa kulinda heshima ya fani na kujikuta wengi wakiangukia katika kashifa na wao kuona ni sehemu ya kujipromoti kumbe jamii inabaki na taswira mbaya kwa wasanii kama ni watu wasio na faida katika jamii.

Tamthilia ya Siri za familia kwa sasa ndio igizo linalotamba na kuwaibua wasanii nyota wengi wenye uwezo kama alivyo Shiffer na kuleta upinzani kwa wasanii wakongwe ambao kwa sasa wamebanwa baada ya soko la filamu kuyumba na kutoa nafasi kwa sinema za nje kuchukua nafasi.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook