Your are here: Home // Habari // SITEGEMEI MWANAUME KUFANYA KAZI ZANGU- AISHA

SITEGEMEI MWANAUME KUFANYA KAZI ZANGU- AISHA

Aisha Bui

Aisha Bui mwigizaji wa Filamu Swahilihood

AISHA Bui mwigizaji wa filamu wa kike Swahilihood amefunguka kwa kusema kuwa yeye katika kuandaa kazi zake za filamu hakuna mchango wowote anaotegemea kutoka kwa mwanaume bali ni kazi ya jasho lake hawezi kuandaa sinema yake na kusubiri hela kutoka kwa Pedeje.

Aisha Bui

Aisha mwigizaji wa filamu Bongo.

Aisha Bui

Aisha katika pozi.

Aisha Bui

Aisha akiwa katika pozi la picha

“Kazi ya utengenezaji wa filamu kwangu naichulia kama sawa na biashara nyingine, hivyo ninavyotengeneza na kutumia pesa yangu si kutoka kwa mwanaume kama wengine wapo hivyo mimi ni tofauti,”alisema Aisha.

Mwigizaji huyo anasema kuwa anapowekeza fedha katika sinema lengo lake kubwa ni kuweza kuzungusha mtaji wake endapo atakuwa akitegemea pesa kutoka mwanaume hawezi kufikia malengo kwani muda wote atataka kumwangalia mwanaume na y eye hataki kuwa tegemezi, ndio maana akatafuta mtaji wake.

Msanii huyo anasema kuwa unapoingia katika kazi yoyote lazima ujipange kwa ajili ya kulinda mtaji wako na kuuendeleza kwa ajili ya kuepukana na utegemezi wa pesa kutoka kwa wanaume wakati wana nguvu na uwezo wa kujitafutia kipato chao.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook