Your are here: Home // Habari // WAKONTA APATA KIFAA MAALUM CHA KUANDIKIA

WAKONTA APATA KIFAA MAALUM CHA KUANDIKIA

Wakonta Kapunda

Wakonta mwandishi wa Script Swahilihood

MWANDISHI wa muswada (Script) mahiri Wakonta Kapunda amesema kuwa anafurahia kila siku zinavyosongea anazidi kupata unafuu wa kuandika kwani hivi sasa kuna rafiki yake ambaye amempatia kifaa maalum kinachomezesha kuandika kazi zake kwa kutumia kifaa hicho toafauti na awali alikuwa akitumia ulimi.

Wakonta Kapunda

Wakonta akiwa na kifaa maalum cha kuandika anachotumia kwa sasa

Wakonta Kapunda

Wakonta akiwa na mito siku za nyuma

Wakonta Kapunda

Wakonta Kapunda

“Kifaa hiki kimetengenezwa kulinga na mahitaji yangu nashukru sana rafiki yangu wa Instragram Hiba Dhiyebi ambaye aliniona katika kipindi cha BBC nikiandikwa kwa shida nikipangiwa mito,”alisema Wakonta.

Wakonta amesema kuwa rafiki yake huyo alimweleza mjomba wake na kumuonyesha jinsi alivyokuwa akiandika na kuweka mito kumsaidia kuandika akitumia ulimi hivyo aliamua kumtengenezea kifaa hicho kwa kumsaidia na kimekuwa msaada mkubwa kwani anasema awali alikuwa akipata shida jasho na uchovu anapooandika muda mrefu.

Akiongelea msaada huo Wakonta amedai kuwa mjomba wa Hiba ni mtaalam wa vifaa mbalimbali kulingana na matumizi ya mhusika kama alivyofanya kwake na kumsaidia kifaa hicho Wakonta ni binti mwenye kipaji cha uandishi wa miswada kwa kutumia Ulimi na kuweza kushiriki katika harakati za utengenezaji wa filamu.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook