Your are here: Home // Habari // GABO ZIGAMBA AZINDUA YAKE FILAMU FUPI YA KISOGO LEO DAR

GABO ZIGAMBA AZINDUA YAKE FILAMU FUPI YA KISOGO LEO DAR

Salim Ahmed

Gabo mwigizaji wa Filamu Swahilihood.

MWIGIZAJI nyota wa filamu Swahilihood Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ amezindua filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Kisogo ambayo inaonekana katika Mobile App Uhondo, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo na kuhudhuliwa na wanahabari mbalimbali na kuweza kushuhudia filamu hiyo.

Salim Ahmed

Gabo akiongea na wanahabari Idara ya habari Maelezo

Salim Ahmed, Aron, Myovela

Gabo leo katika idara ya habari maelezo

Salim Ahmed

Gabo akiwa katika mkutano na wahandishi wa habari

salim

Gabo akiwa katika mkutano

Kampuni ya Sarafu Media chini ya mkurugenzi wake Salim Ahmed (Gabo Zigamba) imekuja na utambulisho wa filamu kubwa na iliyotengenezwa Kimataifa ijulikana nayo kwa jina la Kisogo, filamu hii ambayo ni fupi imejaa weledi wa hali ya juu katika utengenezaji wake lengo ikiwa kufikisha ujumbe kwa katika jamii husika.

Filamu ya Kisogo imelenga kutoa hamasa kwa watanzania kuziona filamu za kitanzania na zile zinazotumia Lugha ya Kiswahili pekee ili kutoa fursa kwa vijana na jamii husika kwa ujumla kutumia njia rahisi na Rafiki ya Simu, filamu zitakazoonyeshwa ni zile zinazotengenezwa na hapa nchini katika kutangaza Lugha yetu nzuri ya Kiswahili kupitia kazi zao ikiwa kampeni ya Sarafu Media kuitangaza lugha hiyo na kuwa ni bidhaa muhimu Ulimwenguni.

“Ni ukweli usiopingika ya kuwa hivi sasa kila Raia awe mjini au kijijini ana uwezo wa kutumia simu ya mkononi kwa mantiki hiyo kwa filamu bora na yenye ujumbe kama ya Kisogo itafikisha ujumbe na kutoa burudani bila upendeleo kwa kila Mtanzania,”

Filamu ya Kisogo itaonekana katika kuanzia leo katika Mobile App ya Uhondo
Mfumo huu utamuwezesha mpenzi wa filamu kuangalia mfululizo wa filamu kali na za kusisimua kutoka kampuni ya Sarafu Media chini ya kiongozi Gabo Zigamba kupitia Mobile App ya Uhondo anatarajia kuibua vipaji na kuvitangaza ikiwa ni njia ya kuwatengenezea ajira.

Pamoja na kuwa mfumo rafiki na wa kipekee katika kuangalia sinema zenye ubora ,Sarafu Media pia itatumia fursa hiyo kuweza kukufanya mpenzi wa filamu kuona filamu zinazorushwa katika Mobile App yao ya Uhondo filamu kutoka sehemu mbalimbali zinazotumia Lugha ya Kiswahili kutoka popote Ulimwenguni.

Mkurugenzi wa Sarafu Media Salim Ahmed amesema kuwa katika kuzingatia maendeleo ya tasnia ya filamu ni lazima kuwe na njia rahisi kwa mtazamaji kufikiwa alipo, mtu ataweza kuangalia sinema ya Kisogo popote alipo kwa kutumia simu yake ya Kiganja kuangalia dakika 15 bure na Dakika 15 zilizobaki utachangia ya kwa gharama ndogo tu Tshs. 500/ na kuona filamu yote.

Gharama hiyo ndogo itasaidia kuweza kutengeneza kazi nyingi na bora ili mtazamaji na mpenzi wa Gabo kuendelea kupata burudani, Elimu kupitia kazi zenye ujumbe mahsusi kama ilivyo sinema bora ya KISOGO,

Lakini ni kazi ambayo imeshirikisha wasanii nyota wengi ambao ni Gabo mwenyewe, Wema Sepetu, Millard Ayo na wasanii wengine wenye vipaji na uwezo mkubwa ambao wamepikwa wakapikika kwa ajili ya kulinda thamani ya fedha yako, sinema ni nzuri sana na mtaweza kuangalia teaser kama sehemu ya kutambua ubora uliopo katika kazi hiyo ya kimataifa kutokea Tanzania.

Kwa kutambua mchango wenu wanahabari tunaamini mtaungana nasi katika kuhakikisha Filamu ya Kisogo inakuwa ni chachu ya maendeleo ya tasnia ya filamu Tanzania, Pia tunaomba ushiriki wenu katika kufanikisha tukio hili.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook