Your are here: Home // Habari // FILAMU YA INNER STRUGGLE KURUKA ZIFF, KUGAIWA BURE

FILAMU YA INNER STRUGGLE KURUKA ZIFF, KUGAIWA BURE

Eva Lundgren

Eva Lundgren mtayarishaji wa Filamu Swahilihood

FILAMU ya The Inner struggle inatarajia kuonyeshwa katika tamasha kubwa la filamu Afrika ya Mashariki la Zanzibar International Film Festival (ZIFF) sinema hiyo ambayo imetengenezwa hapa nchini ikielezea maisha ya watu wenye ulemavu wa Ngozi (Albinisim).

Bethel , Eva Lundgren

Bethel akiwa na Eva Lundgren

Bethel, Eva,

Bethel, Eva Lundgren, Myovela

Bethel, eva

Bethel, akiwa na mtayrishaji wa filamu ya The Inner Struggle

Eva Lundgren

Eva Mtayarishaji wa filamu

Eva akiwa na Bethel katika mkutano na waandishi wa Habari

Eva akiwa na Bethel katika mkutano na waandishi wa Habari

waandishi

Wanahabari wakiwa katika mkutano na mtayrishaji

Sinema ya The Inner Struggle imeelezea maisha ya binti mwenye Albinism ambaye ni yatima na hana msaada kutoka pande nyinmgine huku mama yake akiwa hana uwezo wa kumnunulia lotion maalum kwa ajili ya kujipaka na kuepukana na athari itokanayo na kuungua na jua.

Akiongea na FC mtayarishaji wa filamu hiyo Eva Lundgren Stenbom anafurahia kufanikisha kazi ya utengenezaji wa filamu ya The Inner Struggle kwani itatoa elimu kwa watu wote ulimwenguni kutoa dhana ya kuwatenga na kuwaona kama ni watu toafuti na watu wengine wa kawaida.

“Ninayo furaha kubwa sana kwa kufanikisha utengenezaji wa filamu ambayo inatufundisha kuishi vizuri na watu wenye Albinism kwani watu sawa tu na binadamu mwingine napenda tuwapende,”amesema Eva.

“Mtoto kuzaliwa na Albinism si mkosi, si uchawi ni ukosefu wa madini tu mwilini lazima tuguswe na kuwasaidia kusoma na mahitaji mengine,”

Sinema hiyo imetengenezwa kwa ufadhili wa taasisi kutoka nchini Sweden kwa kushirikiana na Under the Same Sun, lengo kuu kuieleza jamii kuwa mtoto kuwa na Albinism ni ukosefu wa aina ya madini fulani mwilini na si kitu kingine wala si uchawi.

The Inner Struggle imerekodi katika mkoa wa Mwanza na kuongozwa na Mans Ahlin, muongozaji msaidizi Novatus Nago Mgulusi, mtayarishaji Vicky Ntetema, mpiga picha Emmanuel Edward, sauti Ezekiel Mkusa, Mtayarishaji mkuu Eva Lundgren Stenborm.

Waigizaji ni Wambura Mtani, Shasa S Wambura, Marietha Marco, na wasanii wengine kutoka mkoani Mwanza ambao wamefanya makubwa katika filamu hiyo.

Filamu itaonyeshwa katika tamasha la filamu la ZIFF Zanzibar tarehe 15 Julay 2017 siku ya jumamosi, baada ya hapo sinema hiyo itaonyeshwa kupitia mitandao ya kijamii na kuonyeshwa sehemu za wazi pia Dvd na kusambazwa katika taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuelimisha jamii kila kona.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook