Your are here: Home // Habari // SIZAI HADI NDOA KWANZA- DR. SANDRA WA SIRI ZA FAMILIA

SIZAI HADI NDOA KWANZA- DR. SANDRA WA SIRI ZA FAMILIA

Mwajabu Omary

Dr. sandra mwigizaji wa filamu Swahilihood.

MWAJABU Omary ‘Dr. Sandra’ mwigizaji anayetamba katika tamthilia ya Siri za familia amefunguka kwa kusema kuwa pamoja na kuwa na mchumba wake zaidi ya miaka mitano katika mahusiano lakini hawezi kumzalia watoto hadi akimuoa na kufunga ndoa.

Mwajabu Omary

Dr. Sandra katika pozi

Mwajabu Omary

Dr. Sandra mwigizaji wa filamu Swahilihood

Mwajabu Omary

Dr. Sandra katika ubora wake

“Najua mchumba wangu ananipenda sana na nipo nnaye zaidi ya miaka mitano, lakini sitaki kuzaa nje ya ndoa kwani sisi wasanii mara nyingi ndio kioo cha jamii hivyo hutakiwi kukosea hesabu,”

Muigizaji huyo amedai kuwa anatamani kuzaa watoto watatu na kati ya hao wanaume wawili na wa kike mmoja ndio anatakuwa ametimiza ahadi yake, msanii huyo anaamini kuwa umaarufu alio nao kupitia tamthilia hiyo ni kuendelea kuongeza mashabiki kwa kuwa na tabia ya mfano mzuri.

Msanii huyo anasema kuwepo katika kundi la Siri za Familia amejipatia faida nyingi sana ikiwa ni pamoja na kufanikisha biashara zake ambazo wateja wamekuwa wengi kutokana nay eye kuonekana katika tamthilia hiyo ambayo urushwa kupitia Runinga ya East Africa Tv.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook