Your are here: Home // Habari // UMRI WANGU NI WA KUKIMBIA NITAWAKIMBIZA SANA- IBRAH

UMRI WANGU NI WA KUKIMBIA NITAWAKIMBIZA SANA- IBRAH

Ibrahim Osward

Ibrah muigizaji wa filamu Swahilihood

MUIGIZAJI bora wa kiume wa filamu katika tamasha la filamu Zanzibar International Film Festival (ZIFF) Ibrahim Osward ‘Ibrah’ kupitia filamu ya Tunu ametamba kuwa ana nafasi kubwa sana kuzoa tuzo nyingi kulingana na umri wake mdogo kwani wote waliowahi kuchukua tuzo hiyo hawakuwa na umri kama wake.

Ibrahim Osward

Ibrah akisindikizwa kuchukua tuzo ya muigizaji Bora wa kiume ZIFF

Ibrahim Osward

Ibrah akiongea na wadau wa filamu ZIFF

“Namshukru sana Mungu kwa kuniweka juu na kushinda tuzo kubwa ya ZIFF kama muigizaji bora wa kiume kwa mwaka 2017/18 naamini nitawakimbiza sana umri wangu unaruhusu,”alisema Ibrah.

Msanii huyo alikuwa kinara katika filamu ya Tunu ambayo ilirekodiwa kwa ajili ya kuhamasisha vijana kubaki kijijini kujishughulisha na kilimo badala ya kukimbilia mijini na kupata matatizo Ibrah umaarufu wake ulianza siku za nyuma baada ya kuigiza filamu kadhaa kama Popo, Siri ya Mtungi na nyinginezo.

Filamu ya Kumekucha Tunu imerekodiwa Mkoani Morogoro ikitayarishwa na MFID chini ya Director Jordan Riber na kuwashirikisha wasanii nyota kama vile Jacob Stephen JB, Tin White na wasanii wengineo kutoka Morogoro.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook