Your are here: Home // Habari // JOHARI AWAMWAGIA SIFA BONGO MOVIE NIGHT

JOHARI AWAMWAGIA SIFA BONGO MOVIE NIGHT

Blandina Chagula

Johari m,wigizaji wa Filamu Swahilihood.

MUIGIZAJI nyota katika tasnia ya filamu Swahilihood Blandina Chagula ‘Johari’ amewamwagia sifa na pongezi waandaaji wa Bongo Movie Night kwa kuanzisha onyesho la filamu za ndani ambazo kuna wakati zinatoka na kuishia katika Dvd tu kwa ajili ya matumizi nyumbani tu.

Bongo movie night

Wadau wa filamu wakiwa nje katika kupiga picha kabla ya kuingia ukumbini.

Bongo movie Night

wadau wa filamu Swahilihood wakiwa katika picha

Bongo Movie Night

wakifuatilia sinema ya Johari

Glory, Beatrice

Glory msanii wa filamu akiwa na Beatrice mwigizaji rafiki yake.

Blandina chaguila

Johari akiongea na wanahabari hawapo pichani,

z johari 532Akiongea na FC Johari amesema kuwa ni lazima watanzania wawe na uwezo wa kuangalia kazi zilizoandaliwa na watanzania wenzao ambao sinema zao nyingi hazionyeshwi katika majumba ya sinema japo zinaweza kupendwa na watazamaji lakini kutokana na kiingilio kuwa kikubwa wanashindwa.

“Leo nimekumbuka mbali sana tulipotoka na sehemu ambayo tulianza sanaa na kufika hapa, napenda kuwapongeza sana waandaaji wa Bongo Movie Night ni wazo zuri sana linakuza tasnia,”amesema Johari.

Bongo Movie Night uonyeshwa kila Alhamisi ya mwezi ilianza rasmi tarehe 29. June. 2017 na kufanyika kwa mafanikio makubwa, katika onyesho la leo nyota wengi walijitokeza kama vile Biggie, Jafar Makatu, Nkwabi, Side wa Kitonga na wasanii wengine wengi.

Mwalimu Issa Mbura kutoka chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Masoud kaftany, wasanii kutoka kundi la TMT walikuwepo kuangalia sinema ya Johari, huku Johari akiwa ameongozana na Nuru Nassor ‘Nora’ moja ya nyota wakali kabisa Bongo.

Onyesho hili linaandaliwa na Filamucentral chini ya kampuni mama ya Production X, inafanyika katika ukumbi wa BASATA ikisapotiwa na Bodi ya Filamu, Basata ikiwa lengo kuu kuwajengea wadau wa filamu utamaduni wa kuangalia filamu pamoja.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook