Your are here: Home // Habari // FILAMU YA MAGWANGALA YAKWAMA KUZINDULIWA GEITA

FILAMU YA MAGWANGALA YAKWAMA KUZINDULIWA GEITA

Anastazia wambura

Mhe. Wambura Naibu Waziri Wizara ya Habari utamaduni sanaa na Michezo

FILAMU ya Magwangala iliyotarajia kuzinduliwa baada ya kukamilika imekwama kuzinduliwa baada ya kutoke mvutano kati ya watayarishaji na uongozi wa kampuni ya madini ya (GGM) Geita, sinema hiyo ilikuwa izinduliwe na naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura.

filamu ya magwangala

Taarifa kuhusu filamu ya magwangala

Anastazia Wambura

Mhe. Wambura akiwa katika picha akiongelea jambo picha kutoka maktaba.

Taarifa iliyotolewa na kaimu mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali wizara ya Habari utamaduni Sanaa na Michezo inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo kuondoa hisia za ukinzani katika suala la kawaida la mashauriano kati ya Viongozi.

Suala hilo lilimhusu Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura ambaye alifika Mkoa wa Geita Alhamisi iliyopita kwa lengo la kuzindua filamu ya ‘Magwangala’.

Kabla ya uzinduzi huo kufanyika, naibu Waziri alikutana na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Ezekiel Kyunga pamoja na viongozi wa Mkoa na kubadilishana na nao mawazo kuhusu maudhui ya kazi hiyo ya Sanaa.

Katika kikao hicho ilibainika kuwa, yapo malalamiko kutoka kampuni ya uchimbaji Madini ya Geita (GGM) yaliyohusisha filamu hiyo. Hivyo kutokana na malalamiko hayo, Mhe. Wambura kwa busara aliona ni vema kuahirisha uzinduzi wa filamu hiyo, ili kutoa muda wa majadiliano kwa pande zote tatu yaani upande wa Serikali, uongozi wa kampuni ya GGM pamoja na wasanii wa filamu hiyo ya Magwangala.

Mhe. Wambura alielekeza pande zote tatu kukutana tena kwa mara ya pili tarehe 31 Julai, 2017 ili kufikia muafaka.

Wizara imendelea kutekeleza kwa vitendo sera yake ya kuwafikia wadau na inaendelea kuheshimu na kuunga mkono ubunifu unaofanywa na wasanii bila kuathiri mahusiano katika jamii.

Imetolewa na Zawadi Msalla kaimu Mkuu kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook