Your are here: Home // Habari // MAU FUNDI KUINGIA LEO NA FILAMU YA MWALIMU MASEMELE

MAU FUNDI KUINGIA LEO NA FILAMU YA MWALIMU MASEMELE

Masemele film

Filamu ya Mwalimu Masemele ya Mau Fundi

FILAMU ya Mwalimu Masemele iliyotayarishwa na muigizaji nyota Maulid Ally aka Maufundi imeingia sokoni leo na inasambazwa nchi nzima kwa maduka yote ambayo yanauza filamu za kibongo sinema hiyo imeandaliwa mkoani Morogoro lengo la mtayarishaji ikiwa ni kuwaweka pamoja wasanii wote.

Masemele film

Filamu ya mwalimu Masemele

Maulid ali

Maufundi mwigizaji wa filamu Swahilihood.

maulid Ali

Mau fundi akiwa location kurekodi filamu ya Mwalimu Masemele.

Akiongea na FC Mau amesema kuwa filamu hiyo ni nzuri na ina mafunzo kwa jamii huku ikiacha burudani kwa mtazamaji ambaye ana haki kuipata kwani kuna waigizaji mahiri katika filamu hiyo ambao kama walikuwa katika mashindano, Mau anasema wameitendea haki filamu hiyo.

“Muziki huu si wa kitoto maana unakutana na King mwenyewe yaani King Majuto na Prince wake mwenye Mau fundi kuna nini hapo! Lazima watunyooke, filamu hii inasambazwa na Auguster Company ltd,”alisema alisema.

Sinema hiyo imeongozwa na muongozaji Henry Mwakajumba ikishirikisha wasanii kama vile King Majuto, MauFundi, Monica Sizya, Ramia Lulandala, Muki Abdalah, mpiga picha ni Said Dizele na wasanii wengi kibao.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook