Your are here: Home // Habari // MIMI NA MUME WANGU NI RAHA TU – HUSNA

MIMI NA MUME WANGU NI RAHA TU – HUSNA

Husna Chobis

Husna Chobis mwigizaji wa filamu Swahilihood.

MWIGIZAJI wa kike wa filamu Bongo Husna Chobis amesema kuwa msanii ukibahatika kuzaa katika ndoa ni raha sana kwani yeye toka aolewe amejikuta akiongeza marafiki wenye ushauri wa kimaisha tofauti na awali alipokuwa hajaolewa na anafurahia maisha yake na mumewe Ali Seleman ‘Nirrow’ ambaye naye ni msanii.

husna Chobis

husna katika p[ozi la picha

husna chobis

Husna akiwa kistaa zaidi

husna Chobis

Husna muigizaji wa filamu Swahilihood.

“Kiukweli kuzaa ni raha sana hasa ukiwa na mume muelewa kama mume wangu maana kuna watu wanaamini kuwa mkioana wote wasanii hapakaliki mume wangu ni msanii wa Bongo fleva,” alisema Husna.

“Maisha yetu na mpenzi wangu mume wangu ni raha tu, tunalea mtoto wetu ambaye ni star mtarajiwa maana ninavyomuona mwanagu atakuwa msanii wa kimataifa ana swaga hatari,”

Husana ambaye kwa sasa anajulikana mtaani kwao kama mama Othman aka Ochu anadai kuwa mwanaye Othuman au Ochu anaona fahari kuzaa kwani amepiga hatua nyingine katika maisha kwani mara nyingi wasanii wanatazamwa na jamii kama ni watu wa starehe tu hawawezi ulezi wa familia.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook