Your are here: Home // Habari // FILAMU YA T- JUNCTION MAISHA YETU HALISI BONGO

FILAMU YA T- JUNCTION MAISHA YETU HALISI BONGO

Amil Shivji

Amil Shivji mtayarishaji filamu Swahiihood

MTAYARISHAJI wa filamu wa Kimataifa Amil Shivji amesema moja ya kazi yake ni kuwakilisha kundi la watu wa maisha ya kawaida kabisa ambao wanatamani kusema kitu kwa kupitia filamu zake ni rahisi ujumbe kufika kama vile katika filamu yake mpya ya T- Junction iliyoziduliwa Mlimani City.

Amil Shivji , Imani Man

Amil akifanya mahojiano na mwandishi wa habari

amil shivji

Amil akiongea na wanahabari Mlimani City

Prof. Issa Shivji

Prof. Issa shivji akiongea wanahabari

Dr. Harrison Mwakyembe

Dr. Harrison Mwakyembe katika movie premiere Mlimani City

Dr. Harrison Mwakyembe

Waziri wa Habari utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe

Amil Shivji Cece Mlay

Wasanii pamoja muongozaji wa filamu

Bi. Joyce Fissoo, Dr. Mwakyembe

Bi. Fissoo , Dr. Mwakyembe wakiingia ukumbini kuangalia T – Junction Mlimani city.

Katika uzinduzi wake filamu ya T Junction iliacha historia baada ya kuhudhuriwa na Maprofesa na wageni wa kimataifa ambao walifurahia kuangalia sinema kubwa na ya kimataifa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe alimsifia sana Amil kwa kazi.

“Nilikuja kuangalia filamu kiukweli Watanzania tumepiga hatua sikutegemea kuangalia filamu nzuri kama T- Junction sinema ambayo inagusa maisha ya jamii yetu niseme hongera sana,”

“Kupitia filamu unaweza kuwaongelea watu na maisha yao angalia filamu kama T- Junction ni Social commentary ni sinema inayogusa mambo yanayotokea katika jamii yetu vile vile inagusia watanzania wengi wanaoishi maisha ya chini,”alisema Amil.

Ukweli sinema ya T- Junction ni kazi nzuri inayogusia maisha halisi ya Mtanzania kati ya vita vya Machinga na Mgambo wa Jiji ambao kila uchwao ujikuta wapo vitani kwa kufukuzana na Mgambo kuwapiga Raia na hata kuwapotezea maisha yao

Filamu ya imezidi kuonyesha umahiri wa mtayarishaji huyu pale ilipoingia katika tamasha la Filamu Zanzibar ilipotwa tuzo ya filamu bora na muigizaji Hawa Ally akiibuka mshindi bora wa kike Tanzania na ni moja kati ya filamu za Kibongo inayoonyeshwa kwa kiingilio Mlimani city.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook