Your are here: Home // Habari // ASANTE KWA KUNIKUBALI Mh. WAZIRI J. MAKAMBA- SIDE WA KITONGA

ASANTE KWA KUNIKUBALI Mh. WAZIRI J. MAKAMBA- SIDE WA KITONGA

Said Mbelemba , January Makamba

Side wa Kitonga akiwa na Mh. Waziri wa Mazingira January Makamba

STAA wa Series Comedy kali ya Side wa Kitonga Said Bakary Mbelemba aka Side Jangala Junior inayotamba katika Luninga ya E Tv amefurahishwa sana na kukubalika January Makamba-Waziri wa Nchi, Ofisi ya M/Rais, Muungano na Mazingira kupitia Side wa Kitonga ambayo inakimbiza kupitia kituo chako cha Luninga cha E Tv.

Side wa Kitonga

Series Side wa Kitonga

Said Mbelemba

Said aka Side wa Kitonga akiwa katika pozi

Said Mbelemba, January Makamba

Side akiwa katika picha ya pamoja na Mh. January Makamba waziri wa Mazingira

saidi kitonga“Unajua unakutana na mtu mkubwa na waziri mwenye dhamana kama Mh. Makamba na anakukubali kazi yako ni faraja kubwa sana kwangu na inanipa nguvu na deni kuhakikisha simwangushi,”alisema Side wa Kitonga.

Side anafanikisha kuwapatia burudani wapenzi wa Comedy Bongo akiwa na rafiki yake wa karibu Kalombo Amboni, mwanadada Naomi Chuwa wakiwa kazini vijna hawa ni hatari sana katika kuhakikisha wanakupa Elimu na Burudanihili ni chimbuko la Tanzania Movie Talent.

Side wa Kitonga uruka kila siku ya Alhamisi saa 3:00 Usiku na kurudi siku ya Jumamosi saa 6:00 mchana, jumapili, Jumatatu 5:00 Usiku na siku ya Jumatano saa 5:00 Usiku ni kazi inayoandaliwa na kampuni ya Production X ya jijini Dar Es Salaam wataalamu wa utengenezaji wa Filamu, vipindi makala (Documentray) na Production kwa ujumla.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook