Your are here: Home // Habari // MADAME WEMA KUJA NA FILAMU YA HEAVEN SENT

MADAME WEMA KUJA NA FILAMU YA HEAVEN SENT

Wema Isack Sepetu

Wema Sepetu muigizaji Bongo Movie

Kufanya Premiere Leo mlimani City cinema 26. August 2017
MADAME Wema Isack Sepetu amefunguka kwa kusema kuwa ameingia rasmi na kufanya kazi ya uigiza kwa asilimia mia moja kwani kila siku alikuwa akipokea maoni kutoka kwa mashabiki wake kuwa wanamhitaji kumuona akiigiza lakini kwake tatizo lilikuwa mfumo.

Wema Sepetu

Wema katika pozi

Wema sepetu

Wema akingalia mfano wa Mobile App yake

Wema Sepetu

Wema katika Ubora wake

“Kwa sasa sina masihara katika kazi yangu ya kuigiza kwani ninaigiza na kusambaza mwenyewe kwa kutumia Mobile App yangu sipeleki kwa msambazaji na kusubiria maamuzi yake,”alisema Wema.

Wema amesema katika sinema yake amewashirikisha wasanii kama Gabo Zigamba, Neema Ndepanya na Mama Kawele, filamu ya Heaven Sent itazinduliwa kwa kurushwa katika jumba la sinema Mlimani City tarehe 26. August, 2017 na kupatikana katika mfumo huo kwa njia ya simu na kupatikana duniani kote kupitia Mobile app yake.

Onyesho hili litakuwa kwa ajili ya walioalikwa tu baada ya hapo sinema itapatikana katika Mobile App ya Wema kwa gharama ya kawaida kabisa ili kila mpenzi wa filamu na mashabiki wa mwanadada huyo waweze kuipata kwa urahisi kabisa. Sababu iliyomfanya asiigize sana ni kutokana na ubabaishaji wa wasambazaji.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook