Your are here: Home // Habari // SHINDANO LA EUROPEAN YOUTH FILM COMPETITION 2017 YAINGIA UNGWE YA MWISHO

SHINDANO LA EUROPEAN YOUTH FILM COMPETITION 2017 YAINGIA UNGWE YA MWISHO

Mosse Sakar, Tairo

Mratibu wa Shindano la EYFC Mosse Sakar akiongea na wanahabari hawapo pichani.

Shindano la kusaka vipaji la waandaaji filamu chipukizi la European Youth Film Competition (EYFC) imeingia hatua ya lala salama baada ya kuonyesha filamu hizi maeneno mbali mbali jijini Dar es Salaam. Maonyesho haya ya wazi ya filamu yalianzia Mbagala Zakheim, Mwembe Yanga, Biafra Kinondoni na wiki hii inatamatisha ndani ya Taasisi ya Alliance Francaise jijini Dar es Salaam tarehe 2 Septemba 2017.

European Youth Film Competition

Wapenzi wa Filamu wakifuatilia sinema fupi zinazoshindania sinema Bora katika shindano la European Youth Film Competition

Mosse Sakar

Mosse Sakar Mratibu mkuu wa
Shindano la European Youth Film Competition

Mosse Sakar


Mosse Sakar akiongea na wanahabari kuhusu Shindano la European Youth Film Competition

Shindano la European Youth Film Competition ni mwendelezo wa juhudi za Umoja wan chi za Ulaya nchini Tanznaia kuendeleza sanaa nchini Tanzania.

Umoja wa nchi za Ulaya (EU) imekuwa mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya umaskini kupitia maendeleo endelevu nchini Tanzania, hasa kupitia udhamini wa shuguli za utamaduni na ubunifu.

Mwaka 2016, EU ilizindua program maalum ya kudumisha utamaduni na nchi zinazoendelea ili kuwawezesha wananchi wan chi hizi kufurahia tamaduni zao. Programu hii imewezesha kubadilishana mawazo kati Umoja wan chi za Ulaya na nchi zinazoendelea.

Kwa zaidi ya miaka 25, Umoja wa nchi za Ulaya na washirika wake nchini Tanzania wamekuwa wakiandaa tamasha la filamu kila mwaka. Lakini kutokana na mahudhurio hafifu ya wazawa na wananchi watanzania wameamua kuanzisha shindano amablo litawahusu watanzania kwa kuandaa filamu fupi. Lengo la filamu hizi fupi ni kukuza uwezo wa tayarishaji filamu na kuweza kujielezea mada mbali mbali kupitia kazi zao.

Shindano hili la European Youth Film Competition ambalo hadi sasa bado linaendelea liliwahusisha vijana wenye umri kati ya 18 na 35 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

eyfc film

Wadau wakifuatilia filamu katika viwanja vya wazi

eyfc 2017

Short Film zikionyeshwa kwa wadau sehemu ya mwisho ya shindano

Mussa Sakar , Tairo

Mosse Sakar , Tairo kutoka Bodi ya filamu Tanzania

washiriki katika picha ya pamoja

Washiriki wa shindano katika picha ya pamoja.
Shindano la European Youth Film Competition

Mashindano haya yameendeshwa chini ya kauli mbiu: ‘Ukuaji wa idadi ya watu: Je hii ni changamoto au fursa?

Mshindi wa shindano anatarajia kupata zawadi yenye thamani ya Tshs7 millioni, na mshindi wa pili atapata zawadi yenye thamani ya Tshs5million wakat mshindi wa tatu atajinyakulia zawadi yenye thamani ya Tshs3 millioni.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa mashindano haya, Kiongozi wa umoja huo nchini Tanzania Balozi Roeland van de Geer alisema ‘Kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa idadi ya watu hii inaleta changamoto pamoja na fursa katika shughuli za maendeleo.Kuongezeka kwa idadi ya wati tayari umenesha kuwa mzigo kwenye huduma za jamii kama afya, elimu, miundombinu na maeneo mengi kadhaa.
Lakini kwa upande mwingine ongezeko hilo linaleta rasilimali watu kwenye sekta nyingi za uzalishaji kutokan watu kuwa wabunifu na kwa hivyo kuleta ushindani katika utoaji huduma na uzalishaji.
Shindano hili la filamu ni nafasi ya kipkee kwa vijana wa kitanzania kuonnesha ubunifu wao kwenye eneo husika ambalo ni mhimu kwa maendeleo ya Tanzania’ .

Jumla ya washiriki 128 walituma maombi ya kushiriki kwenye mashindano haya na washiriki 30 walichaguliwa kushiriki kwenye warsha maalum iliyowapa darasa kuhusu kanuni za utengenezaji wa filamu hizo pamoja na kuwaelimsiha kuhusu dhana nzima ya ukuaji wa idadi ya watu nchini Tanzania.

Baada ya kuwapa muda wa mwezi mmoja kuandaa kazi zao, jumla ya filamu 15 zilichaguliwa kuingia hatua nyingine. Jukumu la kuchagua filamu hizi ilikuwa chini ya Majaji waliobobea kwenye tasnia ya filamu Richard Ndunguru, Issa Mbura, Amil Shvji, Mr Deepesh Shapriya na Jaji mualikwa Tulanana Buhohela.

Hizi Filamu 15 zimeanza kuonyeshwa maeneo mbali mbali jijini Dar es Salaam na Jumamosi hii ya 26.08.2017 maonyesho yanahamia Uwanja wa Biafra na hakuna kiingilio. Maonyesho haya ya wazi pia inatoa fursa kwa wananchi kupiga kura filamu wanayoipenda. Tayari filamu hizi zimeonyeshwa Mbagala Zakheim (12.08.2017) na Mwembe Yanga (19.08.2017) ambapo imewavutia watazamaji wengi. Wengi waliohudhuria wamepongeza juhudi za washiriki wa EYFC kwa kuja na vitu vipya tofauti na yale yaliozoeleka kwenye Bongo Movie. Baada ya mizunguko hii Filamu 5 zitachaguliwa ili kuingia fainali.

Wasanii waliofanikiwa kutinga hatua ya 15 Bora ni Christine Pande, Cornelius Mwakanjala, Daniel Manege, Dennis Chacha, Dosi Said, Florence Mkinga, Francis Nyerere, Frank Machiya, Freddy Feruzi, Karim Issa Michuzi, Kherry Kafuku, Louis Shoo, Malik Khamis, Rashid Songoro, Taragwa Anthony na Wambura Mwikwabe.

Filamu hii pia inapatikana kwenye kurasa ya mashindano ya YouTube ya European Youth Film Competition. Kuipigia kura filamu uipendayo, watazamaji wanatuma code ya kila filamu kwenda kwenye namba 0746520610.

Fainali ya Mashindano haya yanatarajiwa kufanyika Tarehe 16.09.2017 na watakuwepo watu wote wanaohusika na Tasnia nzima ya Filamu nchini.

Mashindano haya yanaratibiwa na Umoja wa nchi za Ulaya ikishirikiana na Ubalozi wa Uholanzi, Ubalozi ya Ufaransa, Taasisi za Alliance Francaise na British Council ikishirikiana na Bodi ya Filamu Tanzania.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook