Your are here: Home // Habari // HIDAYA NJAIDI AWAFARIJI AKINA MAMA WANAOTESEKA MUHIMBILI

HIDAYA NJAIDI AWAFARIJI AKINA MAMA WANAOTESEKA MUHIMBILI

Hidaya Njaidi

hidaya Njaidi muigizaji wa filamu Swahilihood.

MKONGWE katika tasnia ya Filamu Bongo Hidaya Njaidi ameguswa na maisha na mateso wanayopata akina mama wa wale waliozaa watoto Vichwa vikubwa na Mgongo wazi ambao wanateseka wakihitaji matibabu, hivyo msanii huyo kupitia taasisi yake anaomba kila mwenye kuguswa aungane naye kuwasaidia.

Hidaya Njaidi

Hidaya njaidi muigizaji wa filamu Swahilihood.

Hidaya Njaidi

Hidaya Njaidi katika pozi la picha

“Nimekuwa nikifika katika taasisi ya Moi kwa ajili ya mazoezi ya mkono wangu nimeguswa na mateso ya watoto Vichwa vikubwa na mgongo wazi nimejitoa kuwasaidia kwa nafasi yangu watibiwe,”alisema Hidaya Njaidi.

Mama Njaidi ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa taasisi ya Culture & Woman Advancement Foundation anawaomba waigizaji wenzake na wadau kwa ujumla wake waungane katika kuhakikisha wanapatiwa matibabu sambamba na elimu kwani madaktari wanasema ni ugonjwa unaokingika.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook