Your are here: Home // Habari // CHANNEL YA SINEMA ZETU YAZINDUA TAMASHA KUBWA LA FILAMU 2017/2018

CHANNEL YA SINEMA ZETU YAZINDUA TAMASHA KUBWA LA FILAMU 2017/2018

Elizabeth Michael, Jacob Joseph, Zamaradi Nzowa

Lulu, Jacob Joseph na Zamaradi Nzowa mratibu wa Tamasha la Filamu Sinema zetu International Film Festival

CHANNEL ya Sinema zetu 103 kupitia kituo cha Televisheni cha Azam Tv leo hii mapema wamezindua tamsha kubwa la filamu kwa Afrika Mashariki na zaidi ya filamu 150 zinatarajia kushindania tuzo mbalimbali na kuibuka na ushindi wa kitita kinono cha fedha sambamba na tuzo kwa washindi watakaopatikana kupitia filamu zitakazoshinda, moja ya sababu kuu ni kuhakikisha kuwa tamasha hilo linatangaza Lugha ya Kiswahili kupitia filamu.

Elizabeth Michael

Lulu Balozi wa Sinema zetu International Film Festival

Jacob Joseph, Zamaradi Nzowa

Jacob Joseph Mkurugenzi na Zamaradi Nzowa mratibu wa tamasha

Elizabeth Michael, Jacob Joseph, Zamaradi Nzowa

Lulu, J. Joseph na Zamaradi Nzowa katika kikao na waandishi wa habari hawapo pichani

Prof. Martin Mhando

Prof. Martin Mhando mtaalam wa masuala ya filamu

Prof. Martin Mhando, Elizabeth Michael, Jacob Joseph

Prof. M. Mhando , Lulu na Mkurugenzi wa tamasha Jacob Joseph

Zamaradi Nzowa

zamaradi Nzowa mratibu wa Sinema zetu International Film Festival akiongea na wanahabari Idara ya Habari Maelezo leo asubuhi

Zamaradi Nzowa

Zamaradi Nzowa akiwasikiliza waandishi wa Habari. Leo Idara ya Habari Maelezo.

Moja ya sababu kuu kuanzishwa kwa tamasha la filamu kupitia Channel ya sinema zetu ni kutoa hamasa kwa watengenezaji wa filamu nchini nan chi zinazotumia Lugha ya Kiswahili kuwasogeza karibu watumiaji wa Lugha ya Kiswahili Duniani, kwani ndio Channel ya kwanza pekee katika ukanda wa Afrika ya Mashariki kuonyesha filamu za Kiswahili na kuenzi Utamaduni wetu.

“Tamasha hili litakuwa la kipekee ambalo litafanyika katika Televisheni ili kuongeza thamani ya Utamaduni na Utaifa, vile vile tamasha litakuwa ni jukwaa muhimu litakalojuimusha tasnia nzima na kuinua viwango vya filamu za Kiswahili,”

“Kukua kwa tasnia kunategemea kuwatambua watengenezaji, Wasambazaji na watazamaji, matamasha kama ZIFF yanawafikia watu wachache kwa kuonyeshwa tamasha hili katika Televisheni litawafikia wengi na kupata maoni yao na linakuwa tamasha la kipekee,”amesema Prof. Martin Mhando ambaye ni Jaji mkuu.

Mkurugenzi wa Tamasha hilo Bwa. Jacob Joseph kuwa wamebuni njia maalum ili kuwafikia wadau wa tasnia ya filamu Duniani kote, wakianzia na mfumo wa ukusanyaji wa filamu zitakazoingia katika ushindani kwa hapa ndani ambapo vituo vya kukusanyia ni Morogoro, Zanzibar, Tanga, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na Mtwara. Pia kutakuwa na vituo Nairobi, Kampala, Kigali, Bunjumbura na Goma Mawakala wameshachaguliwa na wanaanza kazi leo rasmi.

“Tunaamini kwa kuwa na vituo vya kukusanyia filamu ambazo zinaingia katika tamasha letu tutawafikia washiriki wote wanaotumia Lugha ya Kiswahili pale walipo na kulifanya liwe tamasha la kipekee zaidi na kuwafikia watengeneza wa filamu wengi zaidi,”amesema Jacob Joseph Mkurugenzi wa Tamasha.

Naye mratibu wa Tamasha hilo Zamaradi Nzowa amesema kuwa nia kuu ya tamasha hili ni kuinua wigo wa tasnia ya filamu Bongo na kuwawezesha watu kuona filamu za Kiswahili zenye maudhui ya Utamaduni wa Kitanzania ambao ndio haswa waongeaji wakuu wa Lugha hiyo inayozidi kusambaa kwa kasi duniani kwa sasa.

“Lengo kuu la tamasha kukuza taaluma ya filamu na kuongeza ubunifu na kutambua ubora na ufanisi katika utengenezaji wa filamu pamoja kuongeza hamasa kwa watazamaji na watengenezaji wa filamu wa filamu za Kiswahili ulimwenguni,”amesema Zamaradi Nzowa Mratibu wa tamasha hilo.

Naye balozi wa Tamsha hilo Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa ni faraja kubwa kwake kwa kuwa balozi wa tamsha hilo kwani anaamini wasanii kama yeye wapo wengi na wangeweza kupatiwa nafasi ya kuwa mabalozi lakini kwa Sinema zetu kumuamini yeye ni jambo nzuri naye atahakikisha kupitia tamasha hilo anaitangaza Lugha ya Kiswahili na kujenga thamani ya filamu za Bongo.

Tamasha hilo linaambatana na utoaji wa tuzo kwa washindi watakaoibuka kidedea kufuatia vipengele vilivyowekwa ambavyo ni

1. Filamu Bora itashinda kitita cha Tshs. 5,000,000
2. Filamu fupi Bora itapata kitita cha Tshs. 2,000,000
3. Makala bora itajishindia Tshs. 1,000,000
4. Muigizaji Bora wa Kiume Tshs. 5,000,000
5. Muigizaji bora wa Kike Tshs. 5,000,000
6. Muigizaji bora wa Komedi Tshs. 2,000,000
7. Muandishi bora wa Muswada filamu 2,000,000
8. Muandishi bora filamu fupi Tshs. 1,000,000
9. Mhariri bora wa filamu Tshs. 2,000,000
10. Mhariri bora filamu fupi Tshs. 1,000,000
11. Muziki bora filamu Tshs. 2,000,000
12. Muziki bora filamu fupi Tshs. 1,000,000
13. Mpiga picha bora wa filamu Tshs. 2,000,000
14. Mpiga picha bora wa filamu fupi Tshs. 1,000,000
15. Mpiga picha Makala Tshs. 1,000,000

Ukusanyaji wa filamu umeanza leo rasmi hadi mwisho tarehe 30. November 2017, sinema zilizopokelewa na kupitishwa baada ya kukidhi vigezo zitaanza kuonyeshwa kuanzia tarehe 1. January 2018, filamu zinazotakiwa kushiriki ni zile zilizotengenezwa kuanzia mwaka 2015, mwezi February 2018 filamu zilizochaguliwa zitaanza kuruka kama washindani na kati ya hizo moja itashindwa kwa kuchaguliwa na watazamaji.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook