Your are here: Home // Habari // SINEMANI YAPAGAWISHA TUKUYU MBEYA, RAI WAFURAHIA FILAMU BORA

SINEMANI YAPAGAWISHA TUKUYU MBEYA, RAI WAFURAHIA FILAMU BORA

Sinemani film Tukuyu

Watu wakiwa makini kuangalia filamu fupi ya Naomba Niseme katika viwanja vya Tandale (Dr. Tulia) -Tukuyu

SINEMANI Tour wiki iliyopita ilitinga Mkoani Mbeya katika viunga vya Tukuyu Rungwe na kuteka na kuonga nyoyo kwa wapenzi na wadau wa filamu pale walipopata bahati kuwa wa kwanza kuangalia sinema zinazoratibiwa na kampuni ya Production X , sinema hizi zina ubora wa hali ya juu zikiwa zimepigwa picha kwa ustadi mkubwa na kusambazwa na mradi uu mpya ujulikana nao kwa jina la Sinemani.

Sinemani Tukutu Mbeya

Wadau wa filamu wakiangalia sinema Tukuyu Mbeya

Sinemani Filamu

Sinemani

Sinemani

Wadau wa filamu wakiangalia sinema uwanjani ujio wa Sinemani Mbeya

Sinemani Bongo

Jinsi Screen ilivyofungwa kitaalam

Sinemani Bongo

Wadau wa filamu wakipata burudani kutoka Sinemani

Sinemani Bongo

Sinemani Tukuyu

sinemani Bongo

Sinemani Night

Akiongea na FC mmoja kati ya maofisa wa Sinemani Seif amewashukru sana wakazi wa Tukuyu kwa kujitokeza kwa wingi na kufurahia filamu kali na za kusisimua katika viwanja vya Tandale ambavyo kwa sasa vitakuwa vikiitwa Tulia Group jina la Naibu Spika Dr. Tulia Ackson huku wakishangilia kwa nguvu wakionyesha kuzikubali kwa ubora.

“Filamu za nyumbani zinapendwa sana kwa hiki nilichokiona hapa katika viwanja hivi na tumetembelea katika vibanda vya kuonyesha Video wametupa changamoto zao sababu ni upatikanaji wa filamu za Kitanzania ni mgumu lakini pia zilizopita zilikuwa na maudhui yanayofanana,”

“Sisi kama Sinemani tumeliona hilo na tunajua watu wanataka nini katika filamu hivyo tutawaletea kazi bora zinazowahusu maisha ya kitanzania yaliyowakilishwa katika ubora wa hali ya juu katika sinema zinazotengenezwa na Production X kama mtayarishaji mkuu,”alisema Seif

Sinemani ni mradi uliolenga kumfikia mtazamaji wa filamu za Bongo pale alipo kwa kumpelekea sinema Bora kupitia katika vibanda vya kuonyeshea video baada ya kubororeshwa na kuweza kutumika na wapenzi wa filamu ambao wataweza kuingia wakiwa na familia zao kwani moja ya changamoto ni ukosefu wa unadhifu wa vibanda vingi sasa Sinemani ibororesha.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook