Your are here: Home // Habari // BONGO MOVIE NI ZAIDI YA BONGO FLEVA SENGA AMPOTEZA DITTO

BONGO MOVIE NI ZAIDI YA BONGO FLEVA SENGA AMPOTEZA DITTO

Senga

Senga muigizaji wa Filamu na Komedi Swahilihood.

Senga asimamisha Tukuyu kwa dakika kadhaa mbele ya Dito
TUKIO hili linanifanya niamini kuwa Bongo Movie haijapotea nan i zaidi ya Bongo Fleva hayo yalitokea katika tamasha kubwa la Kimataifa la Tulia Traditional Dances Festival lilifanyika katika viwanja vya Tandale (Tulia Ground kwa sasa) pale alipoibuka msanii wa vichekesho Bongo Senga na kuhamisha umati wa wapenzi wa sanaa waliokuwa wakifuatilia mashindano.

Senga

Senga mchekeshaji Komedi Bongo

Lameck Ditto

Ditto msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo.

Senga

Senga akiwa amepiga picha na kiongozi wa Wasonjo

Senga

Senga akiingia uwanjani kwa shangwe.

Senga

Senga akiwa na kiongozi Wasonjo

Senga alikuwa amezingirwa na watu wengi huku kila mtu akitaka kupiga naye picha na kusababisha vurugu uwanjani na kutumika nguvu ya ziada baada ya Mc Mwakipesile kuwatuliza kwa kuwaeleza kuwa yupo katika ratiba atawasalimia na kuwa nao pamoja kwa muda wote, Senga alienda kuketi na Rais wa shirikisho Simon Mwakifwamba kisha kwenda meza kuu kwa Naibu Spika.

“Tulieni Senga yupo katika ratiba na atapanda jukwaani kwa ajili ya kutumbuiza ni mzalendo huyu anakumbuka sana nyumbani anashiriki katika shughuli za kimaendeleo ya Tukuyu tumpongeze,”alisema Mc Mwakipesile.

Msanii huyo maarufu ambaye mara nyingi uambatana na mchekeshaji mwezake Pembe alikuwa pekee yake ambapo mtu mmoja alisema kuwa pamoja na msanii wa kizazi kipya Lameck Dito kutangazwa kila mara na Mc kama yupo kwa siku mbili na kuwa atatumbuiza lakini katika tamasha hilo lakini bado hakushitua umati uliofurika katika viwanja hivyo, huku wengi wakitaka kupiga naye picha kwa ajili ya kumbukumbu.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook