Your are here: Home // Habari // TARAGWA ATHONY ATWAA TUZO ZA EUROPEAN YOUTH FILM COMPETITION 2017

TARAGWA ATHONY ATWAA TUZO ZA EUROPEAN YOUTH FILM COMPETITION 2017

Antony Taragwa

Antony mshindi wa tuzo za EYFC 2017

BAADA ya kufanyika mchujo kutoka filamu 15 na kubaki filamu 5 tu kwa ajili ya kuibua mshindi kila mshiriki alipatwa na hofu kwani ushindani ulikuwa umejaa upinzani mkubwa, kijanaTaragwa Anthony na filamu yake fupi ya Animation iitwayo Shida za Uani, anaibuka kidedea katika shindano la kuandaa filamu fupi la European Youth Film Competition lilohudhuriwa na watu mashuhuri mbali mbali, fainali hizo zilifanyika Jumamosi tarehe 16 Septemba 2017 katika ukumbi wa Nyumba ya Makumbusho.

AntonyTaragwa

Antony akiongea na wanahabari baada ya ushindi

Antony Targwa

Antony mtaalam wa Katuni mshindi wa kwanza 2017

Songolo

Kushoto Afisa wa Bodi ya filamu Ndg. Simon akimkabidhi hundi Rashid Songoro mshindi namba mbili EYFC 2017

Majaji Issa Mbura mwenye miwani, Dr. Vicensia Shule , Mwl. Richard Ndunguru

Majaji Issa Mbura mwenye miwani, Dr. Vicensia Shule , Mwl. Richard Ndunguru Chief Judge

Mosse Sakar

Mosse Sakar mratibu wa shindano

Antony Taragwa

Mshindi akipokea mfano wa hundi kutoka kwa balozi

Shindano hili ambalo limechukuwa takribani miezi mitatu liliendeshwa na maudhui ya fursa au changamoto inayosababishwa na ongezeko la idadi ya watu na makazi, hii ilitoa fursa kwa waandaaji wa filamu chipukizi kuonyesha uwezo na umahiri wao wa kuandaa filamu, washiriki waliofanikiwa kutinga tano bora ni Dennis Chacha, Freddy Feruzi, Louis Shoo, Rashid Songoro na Taragwa Anthony.

Anthony Taragwa alishinda kupitia filamu yake ya Shida za Uani na kufanikiwa kujinyakulia zawadi yenye thamani ya Milioni 7, mshindi wa pili ni Rashid Songoro na Filamu yake ya TONE alipewa vifaa vyenye thamani Milioni 5, na mshindi wa tatu ni Fred Feruzi na filamu yake ya Bajaji. Watoto Wangu ya Louis Show ilishinda filamu iliyoshiba maudhui na Watu na Samaki ya Wambura Mwikabe ilishinda filamu iliyopigiwa kura kwa wingi.

Shindano hili la kusaka vipaji la waandaaji filamu chipukizi la European Youth Film Competition (EYFC) imeingia hatua ya lala salama baada ya kuonyesha filamu hizi maeneno mbali mbali jijini Dar es Salaam. Maonyesho haya ya wazi ya filamu yalianzia Mbagala Zakheim, Mwembe Yanga, Biafra Kinondoni na wiki hii inatamatisha ndani ya Taasisi ya Alliance Francaise jijini Dar es Salaam tarehe 2 Septemba 2017.

Shindano la European Youth Film Competition ni mwendelezo wa juhudi za Umoja wan chi za Ulaya nchini Tanznaia kuendeleza sanaa nchini Tanzania, Umoja wa nchi za Ulaya (EU) imekuwa mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya umaskini kupitia maendeleo endelevu nchini Tanzania, hasa kupitia udhamini wa shuguli za utamaduni na ubunifu.

Mwaka 2016, EU ilizindua program maalum ya kudumisha utamaduni na nchi zinazoendelea ili kuwawezesha wananchi wa nchi hizi kufurahia tamaduni zao. Programu hii imewezesha kubadilishana mawazo kati Umoja wan chi za Ulaya na nchi zinazoendelea.

Kwa zaidi ya miaka 25, Umoja wa nchi za Ulaya na washirika wake nchini Tanzania wamekuwa wakiandaa tamasha la filamu kila mwaka. Lakini kutokana na mahudhurio hafifu ya wazawa na wananchi watanzania wameamua kuanzisha shindano ambalo litawahusu watanzania kwa kuandaa filamu fupi. Lengo la filamu hizi fupi ni kukuza uwezo wa utayarishaji filamu na kuweza kujielezea mada mbali mbali kupitia kazi zao.

Shindano hili la European Youth Film Competition liliwahusisha vijana wenye umri kati ya 18 na 35 kutoka Tanzania Bara na Visiwani, Mashindano haya yalieendeshwa chini ya kauli mbiu: ‘Ukuaji wa idadi ya watu: Je hiyo ni changamoto au fursa?

Akiongea wakati wa fainali za mashindano hayo kiongozi wa umoja huo nchini Tanzania Balozi Roeland van de Geer alisema ‘Kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa idadi ya watu inaleta changamoto pamoja na fursa katika shughuli za maendeleo, kuongezeka kwa idadi ya watu tayari umenesha kuwa mzigo kwenye huduma za jamii kama afya, elimu, miundombinu na maeneo mengi kadhaa.

“Lakini kwa upande mwingine ongezeko hilo linaleta rasilimali watu kwenye sekta nyingi za uzalishaji kutokan watu kuwa wabunifu na kwa hivyo kuleta ushindani katika utoaji huduma na uzalishaji, Shindano hili la filamu ni nafasi ya kipkee kwa vijana wa kitanzania kuonnesha ubunifu wao kwenye eneo husika ambalo ni mhimu kwa maendeleo ya Tanzania,” alisema Balozi .

Jumla ya washiriki 128 walituma maombi ya kushiriki kwenye mashindano haya na washiriki 30 walichaguliwa kushiriki kwenye warsha maalum iliyowapa darasa kuhusu kanuni za utengenezaji wa filamu hizo pamoja na kuwaelimsiha kuhusu dhana nzima ya ukuaji wa idadi ya watu nchini Tanzania.

Baada ya kuwapa muda wa mwezi mmoja kuandaa kazi zao, jumla ya filamu 15 zilichaguliwa kuingia hatua nyingine. Jukumu la kuchagua filamu hizi ilikuwa chini ya Majaji waliobobea kwenye tasnia ya filamu Mwl. Richard Ndunguru, Issa Mbura, Amil Shvji, Mr. Deepesh Shapriya na majaji waalikwa Tano bora walipatikana baada ya kazi nzuri ya majaji ambao ni Mwl Richard Ndunguru, Issa Mbura, Amil Shvji, Deepesh Shapriya, na Majaji waalikwa Dk. Vincensia Shule Kantarama Gahigiri, na Tulanana Buhohela kutoka Idhaa ya BBC Swahili.

Filamu 15 zilianza kuonyeshwa maeneo mbali mbali jijini Dar es Salaam na Jumamosi ya kwanza ya 26.08.2017 maonyesho yalifanyika katika Uwanja wa Biafra ilikuwa bure. Maonyesho haya ya wazi pia yalitoa fursa kwa wananchi kupiga kura filamu wanayoipenda. filamu hizi zilionyeshwa Mbagala Zakheim (12.08.2017) na Mwembe Yanga (19.08.2017) ambapo watazamaji wengi waliohudhuria wamepongeza juhudi za washiriki wa EYFC kwa kuja na vitu vipya tofauti na yale yaliozoeleka kwenye Bongo Movie. Baada ya mzunguko Filamu 5 zitachaguliwa ili kuingia fainali.

Mchakato filamu 15 zilichaguliwa

Watayarishaji kumi na tano walifanikiwa kutinga hatua ya filamu 15 Bora ambao walikuwa ni Christine Pande, Cornelius Mwakanjala, Daniel Manege, Dennis Chacha, Dosi Said, Florence Mkinga, Francis Nyerere, Frank Machiya, Freddy Feruzi, Karim Issa Michuzi, Kherry Kafuku, Louis Shoo, Malik Khamis, Rashid Songoro, Wambura Mwikwabe na Taragwa Anthony ambaye jumamosi iliyopita aliibuka kidedea baada kushinda mashindano ambayo ni chachu kwa tasnia ya Bongo movie kufanya vizuri.

Mratibu wa shindano hilo Mosse Sakar amewashukru wadau wa filamu na taasisi zote zilizofanikisha kufanyika kwa shindano hilo, anasema ni hatua nzuri akiamini mabadiliko ya sinema kuingia katika mashindano ya kimataifa lazima ushindani, Mashindano haya yaliandaliwa na Umoja wa nchi za Ulaya, Ubalozi wa Uholanzi, Ubalozi wa Ufaransa, the Alliance Française, British Council na Bodi ya Filamu Tanzania.

Kufuatia mashindano hayo inarudisha imani kwa wapenzi wa filamu Bongo kuwa filamu inapooandaliwa vizuri na watayarishaji kupata elimu ya filamu ni rahisi kuingia katika ushindani wa kimataifa na kutengeneza soko nje ya nchi, pia ijidhihirisha kuwa kuna watengenezaji wa filamu wengi wenye uwezo wakipewa nafasi kutengeneza sinema zinazoweza kuleta upinzani kwa watengenezaji wengine nje.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook