Your are here: Home // Habari // SUBIRINI KADI ZA HARUSI YANGU- TINA

SUBIRINI KADI ZA HARUSI YANGU- TINA

Christina Mroni

Tina muigizaji wa filamu Swahilihood.

CHRISTINA Mroni ‘Tina’ amewataka wapenzi na wasanii wenzake wasubiri kidogo tu watamjua mume wake mtarajiwa pale atakapokamilisha hatua muhimu za kufunga naye ndoa, wala wasiwe na wasiwasi kumjua mpenzi wake huyo ambaye hakuwa tayari kumtaja kwa jina kwani wakati wa kufanya hivyo bado kwake.

Omba film

Filamu ya Omba iliyotayarishwa na Tina.

Christina Mromi

Tina akiwa katika pozi

Tina Mromi na Regine Mromi

Pacha Tina na Regina katika picha

christina mromi

Tina akiwa katika pozi

“Akili yangu inaangalia sana kazi kwa sasa baada ya kupigana kwa nguvu zangu na kusambaza sinema yangu ya Omba na kazi zilizopo jikoni sasa nipo tayari kuzaa na kama unavyoniona Mungu kanibariki na baba wa mtoto mtamjua siku ya harusi,”alisema Tina.

Tina pacha wa msanii Regina Mroni amesema kuwa alikuwa bado hajaamua kuzaa mapema ili kufanikisha malengo yake lakini kwa sasa ameamua na anatarajia kufungua ndoa ya kihistoria punde atakapotangaza na kugawa kadi kwa marafiki na ndugu, kwa sasa Tina ni mjamzito japo hakuwa tayari kumtaja mchumba wake hadharani.

Msanii ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu ya Omba ambayo anaisambaza mwenyewe katika Dvd na mtandaoni kwa kumsapoti unaweza kutembelea mtandao wa www.no-comments.tv unaweza kununua filamu hiyo kwa siku pesa za kitanzania Tshs. 500/ na kwa wiki Tshs. 6,000/ tu unaweza kuwaunga wasanii kwa kununua kazi zao.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook