Your are here: Home // Habari // SEMINA MAALUM KWA WAANDISHI WA PATA MBINU ZA KUUZA SCRIPT

SEMINA MAALUM KWA WAANDISHI WA PATA MBINU ZA KUUZA SCRIPT

Filamu Forum

Semina kubwa Filamu Forum kufanyika mwezi huu 2017

KAMA Waswahili wasemavyo nyumba bora utokana na msingi imara kuifanya isimame vema basi na msingi mkubwa wa filamu ni uandishi bora wa muswada (Script), pia lazima ujue unawezaje kuuza kazi yako kwa kuliona hilo Filamucentral.co.tz kwa kushirikiana na Production X wamekuandalia semina maalum.

Gabo msanii wa filamu bongo

Gabo msanii wa filamu bongo

filamu forum 531

Jb 535Semina hiyo ambayo inajulikana kama Filamu Forum inatarajia kufanyika tarehe 26. October .2017 katika ukumbi wa Basata Ilala na itakuwa kwa siku nzima ambapo shiriki watapata maarifa jinsi gani ya kuuza script baada ya kuandika katika misingi bora ya kiuandishi na kufanya soko kuwa pana zaidi pia kupata mbinu za kuuza Script kwa faida.

“Hii ni fursa muhimu sana kwa waandishi wa muswada kwani tunakwenda kuijengea thamani, tunajua kuwa waandishi wapo wengi lakini changamoto unauza wapi na kwa bei gani kwa mnunuzi?,”alisema mratibu Myovela Mfwaisa.
“Kwani umahiri wa wasanii wetu unatokana na uandishi bora wa Script ndio tunaona ubora wa akina Gabo Zigamba, akina JB wajue pa kununua hizo script,”

Kwa wale ambao wanapenda kushiriki wanatakiwa kujisajili kwa kupiga simu namba 0754 578 730 kabla ya tarehe 23. October .2017 Semina hiyo itakuwa na idadi maalum ili kutoa nafasi na muda kwa wale watakaoshiriki na kujipatia ujuzi na maarifa kwao kwa siku nzima ni vema wanaohitaji kujisajili mapema kabla nafasi hazijamalizika.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook