Your are here: Home // Habari // KALLAGE NA BARAZANI ENTERTAINMENT UJIO UMEKUFIKIA!

KALLAGE NA BARAZANI ENTERTAINMENT UJIO UMEKUFIKIA!

John kallage

John Kallage mkurugenzi wa Barazani Entertainment

Historia inaonyesha kuwa wanaoweza kujenga soko ni wale walio pembeni ya uigizaji na hilo linaoneka hivi sasa kwa miradi inayoonekana inaweza kujenga tasnia ya filamu hapa naongelea SINEMANI na BARAZANI, inawezekana ikawa ndio njia rahisi katika kutatua soko la filamu ambalo limetikisika kidogo.

john Kallage

Mkurugenzi wa Entertainment John Kallage akiwa na baadhi ya wafanyakazi.

Tyeeo Barazani

Jengo la Barazani lilopo Kinondoni

JOHN KALLAGE, JACOB STEPHEN, DR. HARRISON MWAKYEMBE

Dr. Mwakyembe, akiwa na Jb, John Kallage wakiwa katika picha ya pamoja TBC 1

John Kallage

Mkurugenzi wa Entertainment John Kallage akiwa ofisini katika majukumu yake.

FC inamuongelea kijana mtayarishaji na muongozaji mahiri wa filamu na Video za muziki Bongo John Kallage ambaye ameweza kurudisha matumaini kwa wadau wa tasnia ya filamu ambao wengi tulipoteza matumaini baada ya Mdosi kuyumba na kupoteza dira katika suala la uuzaji wa filamu Swahilihood Kallage kwa ujasiri anaibuka na Barazani Entertainment.

Barazani ni mfumo wa kisasa wa kuwasiliana na wateja ambao hawatapata karaha ya kwenda madukani na kuulizia kuna filamu gani imetoka au mpya, nilibahatika kutembelea ofisi za Barazani zilizopo Kinondoni na Kallage kuongelea mfumo mzima unavyofanya kazi wanastahili kupongezwa ni wazo ambalo alilianza muda mrefu.
Hadi leo kufanikiwa na kuwa na timu kubwa ya watendaji ni hatua kubwa sana hasa ukichukulia hali halisi ya maisha yetu wadau wa filamu iliyotawaliwa na kutoaminiana, ujuaji kukosekana kwa upendo na ubunifu, ni vema kumpongeza John Kallage kwa kuwaunganisha pamoja na kurudisha matumaini kwa wanatasnia.

“Kumekuwa na mitazamo tofauti kuna wengine wanasema kuwa Dvd hazitauza wengeine hivi lakini ukisikiliza mambo usiyoyafanyia utafiti unaweza kupotea, kuna wateja wanasema hawataki sinema za Kibongo lakini ukienda na msanii kama JB wanataja sinema zake zote,”alisema Kallage akicheka.

Kallage anasema kuwa mradi huu ambao una ubia wa wadau kama 350 hivi una thamani ya Dola milioni 2 na unatarajia kuanza rasmi kwa kuingiza filamu ya Queen of Maasai ambayo ipo tayari na tayari mfumo upo tayari kufanya kazi kwa nchi nzima,

wanastahili pongezi tunaona thamani ya kupenda vya nyumbani.
Wakati hilo likifanikiwa katika kuhakikisha kuwa unapatikana mfumo mbadala kwa kazi za Kibongo pia kampuni ya Production X ikishirikiana na mtandao huu imetambulisha mradi wake wa SINEMANI 2017 ambao unaonyesha sinema za Kibongo zenye ubora katika Video center zile zile tulizozizoea.

Tumeamua kumpongeza Kallage kutokana na juhudi zake katika kupigania soko ambalo limekuwa na malalamiko mengi kuliko faraja, mkurugenzi wa Barazani alisema kuwa pia yeye ni mmoja kati ya waathirika wa mikataba kandamizi ambayo kwao haipo kwani leseni ya kusambaza filamu Barazani ni miezi 18 tu unarudishiwa na kuisambaza pengine.

Pia ni uwazi wa mfumo husika ambao kila mhusika anapata mgawo wake bila kusumbuana kwa kuambiwa bado haujafikia viwango vya mauzo (Not reach target) na suala la watayarishaji kupoteza haki zao kwa kuuza haki miliki na hakishiriki Kallage anasema kila mdau ni muathirika wa mfumo wa usambazaji Bongo

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook