Your are here: Home // Habari // MAPINDUZI KATIKA USAMBAZAJI T-JUNCTION KURUKA KATIKA NDEGE

MAPINDUZI KATIKA USAMBAZAJI T-JUNCTION KURUKA KATIKA NDEGE

T-Junction film

Filamu ya T- Junction inayoruka katika ndege za Emirates na south African Airways

WATENGENEZAJI wa filamu wa sasa wanazidi kutanua soko la usambazaji wa filamu zetu kwa kila Nyanja, tukio kubwa kabisa na la kufurahisha ni filamu ya T- Junction kufanikiwa kurushwa katika ndege kubwa baada ya kufanikiwa kuingia mkataba na mashirika mawili tofauti ambayo ni Emirates Airways na South African Airways.

Amil Shivji

Amil Shivji mkurugenzi wa Kijiweni Productions na Director wa filamu ya T- Junction

T- Junction film

Ndege ya Emirates Airways

T- junction film

Ndege ya South African Airways kuruka filamu ya T= Junction

T- Junction

Filamu ya T- Junction kuonyeshwa hewani

Filamu ya T- Junction imetengenezwa na Kijiweni Productions chini ya mkurugenzi wake Amil Shivji ambaye pia aliongoza filamu hiyo ambayo toka kuzinduliwa kwake ilianza kwa mafanikio makubwa ni hatua kubwa sana kwani toka kuanza kwa utengenezaji ni kwa mara ya kwanza filamu za Bongo kuonyeshwa katika Ndege zinazomilikiwa na mashirika makubwa.

Kama nilivyosema ni mapinduzi makubwa katika usambazaji wa filamu Swahilihood kwani kila siku mifumo mipya inaibuliwa kwa ajili ya kusambaza filamu na kumfikia mtumiaji, sasa katika Ndege ukija mtaani unakutana na Sinemani mfumo rafiki kwa mtazamaji kuanzia mtaani hadi mlimani City.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook