Your are here: Home // Habari // NILIKIMBIA BONGO ILI NIWE MSANII WA KIMATAIFA- KING MWALUBADU

NILIKIMBIA BONGO ILI NIWE MSANII WA KIMATAIFA- KING MWALUBADU

Athumani Masangula

king Mwalubadu muigiozaji wa filamu Bongo.

MUIGIZAJI na mchekeshaji wa kimataifa kwa sasa Athuman Masangula ‘King Mwalubadu’ amedai kuwa moja ya sababu ambayo iilimfanya ahamie nchini Denmark na amefanikiwa kufanya maonyesho mengi kama mchekeshaji pekee yake pasipokutegemea kuwa na kundi amefanikiwa kwani anapata mialiko kutoka sehemu nyingi za Ulaya na Afrika.

Athuman Masangula

King Mwalubadu akiwa Jukwaani.

Athuman Masangula

KingbMwalubadu kazini

Athuman Masangula

ing Mwaluibadu masanii wa filamu.

“Hapa nilipo nisingefika kama ningekomaa tu Bongo hapa wasanii hatukui kila siku tupo pale pale hakuna challenge, ukiwa Ulaya ushindani ni mkubwa sana na kuchekesha Wazungu si mchezo lakini kwangu wanacheka,”alisema King Mwalubadu.

King Mwalubadu ambaye ameipa jina show yake la Ishu alishafanya tarehe 4. October mwaka huu onyesho London katika ukumbi wa Spencer Football Club Northampton msanii huyo anasema kwa nguvu ambayo walikuwa nayo Ze Komedi hakutegemea kama watakuwa hawana show za live katika kumbi anawashauri wachekeshaji watoke nje kukuza vipaji vyao.
Mwalubadu anapambana na uigizaji huku akiwa amedhamiria haswa kuhakikisha anakuwa mchekeshaji nyota wa kimataifa ambaye ana uwezo wa kufanya kazikwa nguvu zake zote ili kuiinua tasnia na kuzalisha vipaji vya watoto, kama vile KAOLE na makundi mengine ambayo yalikuwepo na kujenga ushindani.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook