Your are here: Home // Habari // TUZINDUE TU FILAMU MAANA NDIO KILICHOBAKI BONGO!

TUZINDUE TU FILAMU MAANA NDIO KILICHOBAKI BONGO!

Bongo Premiere

Bongo movie Premiere

TAKRIBANI miezi nane au tisa sokoni hakuna filamu mpya kila ukipita Mitaani unakutana na filamu za zamani ambazo zimekarabatiwa kwa kuzitengenezea makava mapya, Raia wanalalamika kama wanaibiwa lakini watafanyeje na sisi tumeamua kuwafanya hivyo? Kilichobaki kwetu ni kuzindua sinema zetu kisha kapuni.

Cinemax Tanzania

Ndani ya ukumbi siku ya uzinduzi wa filamu

Mc Pilipilii

Mc Pilipili akiwa na mdau katika Red Carpet

Homecoming

Muigizaji Dan Kijo siku ya uzinduzi wa filamu ya Homecoming

Kiumeni film , Idriss Sultan, Ernest

Ernest na Idriss katika uzinduzi wa filamu ya Kiumeni

Siri ya Moyo Film

Wasanii wa filamu ya Siri ya Moyo katika uzinduzi wa filamu hiyo

Bongo movie Premiere

Bongo movie Premiere

Dr. Harrison Mwakyembe, Joyce Fissoo

Mwakifwamba, Rado, Dr. Mwakiyembe na Bi. Fissoo katika uzinduzi wa filamu ya Bei Kali

Hamisa Mobetto, Allan upamba

Filamu ya Zero Player iliyozinduliwa ijumaa

Hiyo inkuwa ni tofauti sana na zile nchi zilizoendelea unapoona inafanyika premiere ujue kesho sinema inaonyeshwa siku inayofuatia kwa maana katika majumba ya sinema popote duniani, sisi hatufanyi hivyo hadi sasa ni filamu nne tu kama sikosei ambazo kiukweli zilikidhi hilo la kufanyika kwa premiere kisha kuendelea kuonyeshwa kwa kiingilio ikiwa ndio hatua kubwa katika usambazaji.

Filamu ya kwanza kabisa kufanya hivyo ilikuwa ni CPU iliruka katika ukumbi wa Century Cinemax Mlimani City mwaka 2010, zikafutia sinema za Kiumeni, T- Junction hizi zote zilionyeshwa kwa kiingilio na watu walilipia kuziona ni hatua nzuri katika kutafuta njia mpya katika usambazaji lakini hizi nyingine ambazo zinazinduliwa tu inakuwaje?

Katika harakati hizo kumbi rafiki inaweza kuwa ni ukumbi wa Cineplex Cinema uliopo Quality centre ambao umekuwa ukitoa fursa kwa baadhi ya makapuni kuonyesha sinema kwa kiingilio bila masharti magumu kama vile ukumbi wa Century Cinema ambao unatakiwa kulipia kwa kununua viti na si wao kuuza na kumlipa mwenye filamu.

Filamu zilizozinduliwa ni nyingi kwa sasa katika sehemu tofauti tofauti hata huko mikoani matukio kama haya yanafanyika sana na viongozi wetu kushiriki na kufurahia lakini baada ya hapo hatuuzi wala mtaani mashabiki zetu hawazioni kwa sababu mara nyingi wafikao katika premiere ni waalikwa tu kwa kadi maalum.

Matukio haya yana umuhimu sana pale tunapofanikiwa kufika kwa wateja wetu kwani kiukweli mikakati ya kiutangazaji haifanyiki basi tunahitaji mifumo ya kiusambazaji kukua zaidi na kuanza chini kabisa kama vile Sinemani ambao wao wanaonyesha filamu za kitanzania katika mtaani kabisa katika majengo yaliyobororeshwa.

Ijumaa iliyopita filamu nyingine inazinduliwa katika ukumbi wa Cineplex cinema ni sinema ya Zero Player iliyomshirikisha msanii wa kike Hamisa Mobetto, lakini hatujui kama itaingia mtaani na kuwafikia wateja umuhimu wa kuwa na majumba ya sinema ya hadhi yetu ni muhimu ujio wa Sinemani ni ishara njema kwa watayarishaji.

Mradi huo unatarajiwa kuzinduliwa katika viwanja vya Biafra tarehe 8 .December . 2017 na tarehe 29. December 2017 kwa kuangalia sinema kubwa mbili T- Junction na Ni Noma wadau wawepo na kuangalia filamu za kiwango hiyo itakuwa mwisho wa kuzindua filamu na kuzifungia ndani.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook