Your are here: Home // Habari // PREMIERE YA FILAMU YA USIJISAHAU KUTIKISA DAR NA ZANZIBAR

PREMIERE YA FILAMU YA USIJISAHAU KUTIKISA DAR NA ZANZIBAR

Issa mussa

Cloud 112 muigizaji wa filamu Swahilihood.

FILAMU ya Usijisahau iliyotayarishwa na muigizaji mkongwe Bongo Issa Mussa ‘Cloud 112’ inatarajiwa kufanyiwa Premiere Dar na Zanzibar mwezi wa December imefahamika, sinema ya Usijisahau imerekodiwa nchini Sweden na kuwashirikisha wasanii wa Bongo ambao ni Wastara Juma na Suleiman Barafu.

Suleiman Barafu Wastara

wasanii Barafu na Wastara wakiwa Sweden kwa ajili ya sinema ya Usijisahau

Issa mussa

Cloud 112 akiwa katika kava la filamu ya Usijisahau

Samia Suluhu, issa mussa

Cloud 112 akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan

Issa Mussa , mama Samia Suluhu

Cloud 112 akiongea na Mh. Samia Makamu wa rais kuhusu mikakati ya Premiere nchini Tanzania.

“Tuaamini filamu yetu itatikisha na kuacha gumzo katika premiere Dar na Unguja yaani Zanzibar kwani kwa muda wote nilioishi nje ilikuwa kwa kazi moja tu kuhakikisha nafanya kitu cha kipekee nimeamua kuipa heshima nchi yangu kwanza,”alisema Cloud.

Cloud ameiambia FC kuwa premiere itaanza kufanyika Jijini Dar es salaam tarehe 2. December .2017 katika ukumbi wa Century Cinema Mlimani City na tarehe 8. December . 2017 watakuwa Ngome kongwe katika harakati za kuwapa nafasi mashabiki wa filamu Zanzibar na sehemu zingine za Bongo kisha nje ya nchi ikiwa ni sehemu ya kutanua soko la filamu.

Msanii huyo amekuwa ni balozi mzuri katika Lugha ya Kiswahili kupitia filamu kwani akiwa huko amefanikiwa kurekodi filamu na kuwashirikisha wasanii wa nchi mbalimbali kwa kutumia Kiswahili na amefanikiwa kuongea na viongozi Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Mwakyembe.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook