Your are here: Home // Habari // TUFANYE KAZI BORA KUTEKA SOKO LA AFRIKA – BI FISSOO

TUFANYE KAZI BORA KUTEKA SOKO LA AFRIKA – BI FISSOO

joyce Fisssoo

Bi. Fissoo katibu wa Bodi ya filamu Tanzania

KATIBU mtendaji wa Bodi ya filamu Bi. Joyce Fissoo amewashauri wadau wa filamu kuongeza ubora katika utengenezaji wa filamu zetu Tanzania kwani soko linaonekana lipo wazi na sinema za Kiswahili zina nafasi kubwa katika soko la filamu hasa zile nchi zinazoongea Lugha ya Kiswahili na idadi ya waongeaji inazidi kuongezeka.

Joyce Fissoo

Mama Fissoo akiwa katika pozi la picha

Joyce Fissoo

Bi. Fissoo akiongea na wadau

joyce Fissoo

Bi. Joyce Fissoo akisisitiza jambo

Endapo ubora wa filamu utakuwa wa juu sana basin i wazi kuwa sinema kutoka Bongo zitashika soko Ulimwenguni na kuwa nchi pekee inayotumia vema Lugha ambayo inakua kwa kasi na kupendwa na watumiaji wengi sana kwa sasa, lakini Bongo Movie ni jina lilokubalika kama alama ya tasnia ya filamu kama Hollywood, Bollywood na Nollywood.

“Wadau wa filamu tujitahidi sana kutengeneza kazi zenye ubora kwani kwa sasa inakadiliwa watu wanaozungumza Kiswahili ni zaidi ya wazungumzaji milioni 150 sinema zetu zikitumika vizuri ni soko pana sana kwetu,”alisema Bi. Fissoo.

Katibu ametoa rai hiyo baada ya kuhudhuria mkutano mkubwa wa filamu Nairobi nchini Kenya uliojulikana kwa jina la International Film Convention 2017 ambapo katika mjadala Tanzania imetambuliwa kuwa ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa filamu Afrika baada ya nchi ya Naijeria huku ikiwa bado haijalifikia soko kubwa kote Ulimwenguni,endapo sinema zetu zikiandaliwa kwa ubora soko ni kubwa.

Hadi sasa filamu za Kiswahili zinazalishwa kwa wingi Tanzania pekee kwa Afrika mashariki, na kuwa ndio mtaji mkubwa sana na alama inayoitangaza tasnia hiyo kwani Lugha ya Kiswahili inatumika katika sinema nyingi na kwa sasa kutokana na utendaji mahiri wa katibu wa Bodi ya filamu Bi. Fissoo filamu inatambulika katika majukwaa makubwa ya filamu Ulimwenguni.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook