Your are here: Home // Habari // WABONGO WANAPENDA SANA NGONO- SISTER FEY

WABONGO WANAPENDA SANA NGONO- SISTER FEY

Faidha Omary

Sister Fey muigizaji wa filamu na muziki

BAADA ya kutikisa na video za kustaajabisha katika mitandao ya kijamii mwanadada Faidha Omary ‘Sister Fey’ amefunguka kwa kusema kuwa yeye yupo makini na hajafanya kama mwanamke mhuni bali alikuwa yupo kazini na hayo si maisha yake yeye ni mtu anayejiheshimu sana na hayo ni maisha ya sanaa tu.

Faidha Omary

Sister Fey akiwa katika pozi la Taulo moja

Faidha Omary

Sister Fey akiwa katika pozi la kiti

Faidha Omary

Sister Fey katika ubora wake

Msanii huyo ambaye amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii hivi sasa baada ya kuposti video za kupagawisha kwa kupiga video ya kwanza akiwa mapaja wazi na kusema kuwa anablid kisha kukaa katika dishi la maji akiwa kajifunika taulo, ni ujio tu wa wimbo wake kaja mwenyewe, anatafuta mashabiki tu.

“Nilikuwa gizani toka mwaka 2016 nikifanya kazi zangu na wanaofaidika wengine, wanaposti kazi zangu bila idhini yangu na nikitoa wimbo kimya filamu kimya nikajiuliza nikagundua watu wanapenda sana ngono,”alisema Sister Fey.

“Na kweli nilipoposti video ya kwanza kama nablidi tu na mapaja nje nimepata folowazi wengi sana Wabongo hawataki vitu vya kuumiza kichwa wawekee picha za mambo hayo utawakusanya,”

Msanii wa filamu na muziki anasema alipoweka video akiwa mapaja wazi huku akisema kuwa yupo katika siku zake alipata folowazi wengi sana na kuamini kuwa watanzania hawapendi vitu muhimu bali ukitaka kuwapata ongelea ngono au vitu vinavyoashiria ngono, aidha anasema kuwa kwa sasa kitu kinacholipa kwake ni muziki, filamu inalinda jina lake.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook