Your are here: Home // Habari // MAADILI YAZINGATIWE KATIKA FILAMU – MH. SHONZA

MAADILI YAZINGATIWE KATIKA FILAMU – MH. SHONZA

Juliana Shonza

Naibu waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh. Juliana Shonza

NAIBU Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza ameitaka Bodi ya filamu kusimamia maadili katika filamu zinazotengenezwa nchini kwani zimekuwa zikilalamikiwa sana kutokana na mavazi mambo ambayo si maadili ya Kitanzania ni wajibu wa taasisi husika kuhakikisha maadili yanalindwa.

Josefina Joseph

Fina Joseph muigizaji wa filamu akiwa katika uvaaji ambao unapingwa.

Joyce Fissoo, Juliana Shonza

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Juliana akimsikiliza kwa makini Katibu Bi. Fissoo.

Juliana Shonza

Mh. Juliana Shonza Naibu waziri wa Habari UtamaduniSanaa na michezo.

“Napenda kutoa rai kwa bodi ya filamu kusimamia filamu zetu ziwe na maadili zisitolewe tu bila kuhakikiwa zikiwa na maadili hatuwezi kuwa na filamu zisozo na maadili yetu na zikaruhusiwa ziingie mtaani,”alisema

Naibu waziri amaesema atakuwa mkali kuhusu suala la maadili kwani filamu hizi zina uwezo wa kufika mbali na kueneza mambo ambayo yanapotosha jamii na kuharibu Taifa ni vema kuwa na kazi ambazo zitatoa mafunzo kwa jamii nzima zitumike kuleta maendeleo kwa jamii na pia ajira kwa watanzania.

Aidha alimpongeza katibu mtendaji Bi. Joyce Fissoo wa Bodi ya filamu kwa kuwasilisha utendaji wa Bodi ya filamu kwa umahiri na Mh. Shonza kujikuta sehemu ya maswali aliyopanga kuuliza yakiwa yamejibiwa kwa ufasaha kabla ya kuulizwa jambo ambalo limeonyesha uwezo na uchapa kazi kwa Bi. Fissoo ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa wadau wa filamu katika ukuaji wa tasnia hiyo.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook