Your are here: Home // Habari // NIPO TAYARI KWA AJILI YA MWAKANI – GABO

NIPO TAYARI KWA AJILI YA MWAKANI – GABO

Salim Ahmed

Gabo Zigamba muigizaji wa filamu Bongo.

SALIM Ahmed ‘Gabo Zigamba’ amejipanga kwa ajili ya mwakani kuja kivingine anasema amekuwa akipata maombi mengi na maoni kutoka kwa wapenzi wa kazi zake kuwa mbona haonekani katika filamu mpya lakini kwake ilikuwa ni vema kujipanga na kuja na kitu tofauti ili mashabiki zake wafurahie kazi zake.

Salim Ahmed

Gabo Zigamba katika suti kali,

Ahmed Salim

Gabo Zigamba akifurahia jambo pichani .

“Kama kawaida yangu napenda kuwa na maneno machache lakini vitendo vingi tena katika ubora mkubwa sasa mwaka ndio unamalizika ni bora tuupishe na tuamke nao January mwaka 2018 tukirudi vitu bora,”alisema Gabo.

Gabo anasema kuwa kuanzia mwakani atakuwapatia kazi zenye kuelimisha huku pia akisema kuwa amejiongeze kwa kufanya tamthilia ijulikanayo kwa jina la Kapuni na anabadili jina kidogo na kuitwa kwa kizungu kama Mr. Brown tamthilia hiyo itaanza kuonyeshwa katika televisheni mwezi wa kwanza Maishabongo magic.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook