Your are here: Home // Habari // SIDE WA KITONGA MSIMU MPYA NI NOMA- NAOMI

SIDE WA KITONGA MSIMU MPYA NI NOMA- NAOMI

Naomi Chuwa

Naomi mchekeshaji na muigizaji wa filamu Swahilihood.

Ujio wa msimu mpya wa simulizi za kusisimua za Side wa kitonga ambayo uruka katika luninga ya E tv zinatarajia kuwa kubwa sana kutokana na mwitikio wa watazamaji na watayarishaji kupokea maoni yao na kuyafanyia kazi mmoja kati ya washiriki wa kundi hilo mwenye uchu wa kuwa muigizaji na mchekeshaji wa kimataifa nao amebainisha hilo.

Naomi Chuwa

Naomi muigizaji wa filamu Swahilihood.

Naomi Chuwa

Naomi akiwa katika pozi

Kalombo, Naomi Chuwa, Said Bakary

Kalombo, Naomi na Side wakiwa katika picha ya pamoja.

Muigizaji na mchekeshaji Naomi Chuwa wa kundi la Side wa Kitonga amesema kuwa malengo yake ni kuwa mahiri kama mchekeshaji na mwanamuziki wa Marekeni Queen Latifa, kwani kwa sasa hapa Bongo haoni mtu wa kujilinganisha naye kwa wachekeshaji wa kike ambao mara nyingi wanashindwa kusimama wao kama wao.

“Kuigiza kwangu ni kazi ambayo nina malengo nayo makubwa sana ninatafikia nafasi kama muigizaji wa kimataifa Queen Latifa ninafanya vizuri katika komedi na baadae kufanya muziki kwa sababu nina kipaji hicho,”alisema Naomi.

“Msimu wa pili wa Side wa Kitonga utakuwa ni Noma kwani tumejipanga hatari kwa ajili ya kuwapa vitu adimu wapenzi wa kazi zetu tupo kikazi zaidi hakikisha haukosi kukaa katika tv yako ya E Tv kila Alhamisi saa 3 usiku,”

Naomi anasema kuwa wachekeshaji wa kike wanashindwa kujijenga kama wanaume ndio maana kila mara utakuta wanaovuma ni wachekeshaji wa kiume tu, yeye ndio anafungua njia kwa wanawake Naomi ni msichana pekee katika kundi la Side wa Kitonga linarusha mchezo wake katika televisheni ya E tv kundi la watu watatu Said Bakary, Kalombo na mwanamke mmoja ambaye ni Naomi.

Wasanii hawa ni moja kati ya zao bora kabisa la vijana waliopata bahati ya kupikwa na Tanzania Movie Talent (TMT) mradi wa kutafuta vipaji uliofanikiwa sana kuzalisha wasanii waliopikika kutoka kwa walimu wenye weledi na ujuzi wa masuala ya filamu na Sanaa kwa ujumla kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook