Your are here: Home // Habari // NINA MVUTO BONGO MOVIE WAJIPANGE- PRETTY KIND

NINA MVUTO BONGO MOVIE WAJIPANGE- PRETTY KIND

Susan Michael

Pretty Kind muigizaji wa filamu Swahilihood.

MSANII chipukizi katika tasnia ya filamu Bongo Susan Michael ‘Pretty Kind’ ametamba kwa kuwaeleza kuwa wasanii wa kike wajipange kwani amefungua mwaka kwa kuingia katika tasnia hiyo akiwa na vitu muhimu ambavyo anaamini atawafunika na kuwa muigizaji wa kike pekee mwenye mvuto na muigizaji bora.

Susan michael

Pretty Kind msanii wa filamu.

Susan Michael

Pretty Kind msanii wa filamu na muziki.

Suan michael

Pretty Kind muigizaji wa filamu Swahilihood katika pozi la picha.

“Sijaingia katika fani ya kuigiza kwa kukurupuka no nimeangalia vitu vingi sana, katika sanaa yoyote na hasa uigizaji lazima uwe na sura ya mvuto umbo la kibantu ambalo bongo movie simuoni kama mimi, wanajaribu kunifananisha sijui Wema mara Kajala mimi ni mimi tu,”alitamba Pretty Kind.

Msanii huyo anasema kuwa anajiamini kuwa yupo tofauti na uwezo wake wa kuigiza ni wa kipekee pia ana umri mdogo ana uhakika wa kudumu zaidi katika gemu pamoja na kuigiza akiingiza kama muigizaji mkuu katika filamu ya Kilio cha mnyonge pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya lakini anaona katika filamu nafasi yake ni kubwa sana.

Pretty Kind pia anatamba na wimbo wake wa Vidudu washa ambao amemshirikisha msanii wa kike mwezake Giggy Money ni matarajio yake kuwa mwaka huu 2018 anauanza vizuri kwa sababu ndio kwa mara ya kwanza anaachia filau yake, kamshirikisha Mama Kawele, Hemed Phd na wasanii wengine wakali Bongo movie.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook