Your are here: Home // Habari // USIKUBALI SHETANI AKUHARIBIE 2018- ODAMA

USIKUBALI SHETANI AKUHARIBIE 2018- ODAMA

Jennifer Kyaka

Odama muigizaji wa filamu Swahilihood.

JENNIFER Kyaka ‘Odama’ muigizaji wa filamu Bongo amewashauri watu kuwa na maamuzi yao kuhusu ndoto na malengo yao pasipo kuangalia au kufuata mipango yaw engine, kwani hiyo ni sawa na kuingiliwa na Shetani na mtu kujikuta akitenda mambo yasiyo na faida kwake na kujikuta mhusika akijutia kwa matokeo ya alichofanya.

Jennifer Kyaka

Odama mtayarishaji wa filamu Bongo

Jennifer Kyaka

Odama akiwa katika pozi la picha.

JKennifer Kyaka

Filamu ya Mr. kiongozi ya Odama.

Jennifer Kyaka

Odama katika pozi

“Usikubali Shetani akuharibie yale uliyoyapanga kwa muda mrefu eti kwa sababu tu wewe pia unataka kufanya waliyoyafanya wengine nakushauri shikilia hapo hapo Sheteni ni muongo, ni tapeli hana ni nzuri nawe,”

Odama anaamini kuwa katika maisha na utafutaji kuna changamoto nyingi sana ambazo ikiwa kama ni vikwazo ni muhimu kuvuka vikwazo hivyo kwa kuamini hisia zako ili uweze kufikia ndoto zako na malengo uliyojipangia mwenyewe ulijipangia kwa muda mrefu na usiwe mtu wa kukatishwa tamaa na wanaokuzunguka.

Aidha Odama ameanza mwaka mpya kwa neema baada ya kuachia filamu ya mpya ya Mr. Kiongozi katika mfumo mpya wa usambazaji sinema yake inasambazwa na kampuni ya Max Malipo kwa bei ya Tshs. 5,000/ tu na inapatikana kwa mawakala wote wa Max Malipo nchi nzima.

filed under: Habari

Leave a reply

Home | About us | Contact us| Privacy Policy | Terms of use | Copyright © 2010 swahili hood portal . All rights reserved.
  • Facebook